Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Wana-Farasi Wanne Katika Mwendo!
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • “Na wao walipewa mamlaka juu ya sehemu ya nne ya dunia, kuua kwa upanga mrefu na kwa upungufu wa chakula na kwa tauni yenye kufisha na kwa hayawani-mwitu wa dunia.” (Ufunuo 6:8b, NW)

  • Wana-Farasi Wanne Katika Mwendo!
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 29, 30. (a) Kungekuwa na tumizi gani leo la yale ‘matendo manne yenye kudhuru’ ya Ezekieli 14:21? (b) Sisi tuelewe nini kwa usemi “hayawani-mwitu” wa Ufunuo 6:8? (c) Ni nini linaloonekana kuwa jambo kuu la mandhari hiyo ya kiunabii?

      29 Njozi ya Yohana hutaja hayawani-mwitu kuwa kisababishi cha nne cha kifo cha mapema. Kweli kweli, hivyo vitu vinne vilivyoonyeshwa kwa kufunguliwa kwa kifungo cha nne—vita, njaa, ugonjwa, na hayawani-mwitu—vilionwa katika nyakati za kale kuwa visababishi vikuu vya kifo cha mapema. Hivyo vingetangulia kuweka kivuli cha visababishi vyote vya kifo cha mapema leo. Ni kama vile Yehova alivyoonya Israeli: “Ndivyo, vilevile, itakuwa wakati kutakuwa matendo yangu manne yenye kudhuru ya hukumu—upanga na njaa na hayawani-mwitu wenye kudhuru na ugonjwa wa kipuku—ambayo mimi hakika nitapeleka juu ya Yerusalemu ili kukatilia mbali kutoka hilo mwanadamu wa dunia na mnyama wa nyumbani.”—Ezekieli 14:21, NW.

      30 Si mara nyingi ambapo vifo vinavyoletwa na hayawani-mwitu vimekuwa vichwa vikuu magazetini katika nyakati za ki-siku-hizi, ingawa katika nchi za kitropiki wanyama-mwitu wamezidi kudai majeruhi. Katika wakati ujao, huenda wakadai hata zaidi ikiwa mabara yanaachwa ukiwa kwa sababu ya vita au watu wanadhoofishwa mno na njaa wasiweze kufukuzia mbali wanyama wenye njaa. Kwa kuongezea, kuna binadamu wengi sana leo ambao, kama wanyama wasiofikiri, wanaonyesha mielekeo ya kihayawani tofauti kabisa na ile inayoelezwa kwenye Isaya 11:6-9. Watu hawa ndio sana sana walio na daraka la mweneo wa pote katika tufe wa uhalifu unaohusiana na ngono, uuaji-makusudi, uvamizi-haramu, na milipuko ya mabomu katika ulimwengu wa ki-siku-hizi. (Linga Ezekieli 21:31; Warumi 1:28-31; 2 Petro 2:12.)

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki