-
Wakutana kwa Njia ya Pekee Baada ya Miaka 30Amkeni!—2002 | Oktoba 22
-
-
Mark Ruge, mwenye umri wa miaka 20, alitoka Buffalo, New York. Alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa taaluma ya ujenzi.
Wakati huo, ilionekana kana kwamba urafiki wao ungalikuwa wa muda mfupi tu. Hakuna yeyote kati yao aliyeendelea na elimu ya chuo kikuu; kila mmoja aliacha masomo na kufuatia mambo mengine. Miaka zaidi ya 30 ikapita. Kisha, siku moja wakakutana tena uso kwa uso katika Jamhuri ya Dominika. Walikutana ghafula na bila kutarajia. Lakini kuna jambo jingine lililofanya wakutane. Ni jambo gani hilo? Ili kupata jibu, hebu tuchunguze maisha ya kila mmoja wao.
-
-
Wakutana kwa Njia ya Pekee Baada ya Miaka 30Amkeni!—2002 | Oktoba 22
-
-
Mark Aunga Mkono Harakati za Kupinga Vita
Mark aliendelea kusoma kwenye chuo kikuu kwa mihula kadhaa baada ya Dennis kuacha, lakini baadaye akaamua kutounga mkono mfumo uliokuwa ukiendeleza vita. Kwa hiyo alirudi Buffalo, ambako alifanya kazi kwa muda akiwa msimamizi kwenye kiwanda cha kutengeneza chuma. Bado hakufurahia shughuli za kivita, kwa hiyo aliacha kazi yake, akanunua pikipiki, kisha akasafiri hadi San Francisco, California. Dennis na Mark walikuwa San Francisco wakati uleule lakini hakuna yeyote kati yao aliyejua hivyo.
Mark alifuga ndevu na nywele ndefu kama Dennis na akaanza pia kuvuta bangi. Lakini Mark alishiriki sana katika harakati za kupinga vita kwa kuunga mkono maandamano ya kupinga vita. Alikuwa akisakwa sana na shirika la upelelezi la FBI kwa sababu ya kukataa kujiunga na jeshi, kwa hiyo kwa miaka kadhaa alitumia majina bandia ili aepuke kukamatwa. Aliishi maisha ya kihuni huko San Francisco. Kisha mwaka wa 1970, Mashahidi wawili wa Yehova wakamtembelea nyumbani.
Mark asimulia: “Nadhani waliona kwamba ninapendezwa, kwa hiyo wakarudi. Sikuwa nyumbani waliporudi, lakini waliacha Biblia yenye rangi ya kijani-kibichi na vitabu vitatu.” Hata hivyo, Mark alijishughulisha mno na harakati za kisiasa na kuponda raha asiweze kupata wakati wa kuvisoma. Wakati uleule alikuwa akisakwa na wapelelezi wa FBI. Alitumia jina jingine bandia, akahamia Washington, D.C. Akiwa huko alianza kuishi na rafikiye msichana aliyeitwa Kathi Yaniskivis, ambaye walikuwa wamekutana kwenye chuo kikuu.
Hatimaye, mwaka wa 1971, wapelelezi wa FBI walimkamata Mark. Wapelelezi wawili wa shirika hilo waliandamana naye katika ndege kutoka Washington, D.C., hadi New York na kuhakikisha kwamba amefika Toronto, Kanada. Inaonekana wapelelezi wa FBI hawakudhani kwamba alikuwa hatari kwa jamii; lakini walitaka tu aondoke nchini. Mwaka uliofuata, yeye na Kathi walifunga ndoa, wakahamia kwenye Kisiwa cha Gabriola, huko British Columbia, Kanada. Walitaka kuishi mbali na watu wengine, lakini walihisi kwamba ni lazima maisha yawe na kusudi.
-
-
Wakutana kwa Njia ya Pekee Baada ya Miaka 30Amkeni!—2002 | Oktoba 22
-
-
Wakati huohuo, Mark na Kathi waliokuwa wakiishi kwenye Kisiwa cha Gabriola, waliamua kuichunguza Biblia kwa sababu walikuwa na wakati. Walianza kusoma tafsiri ya King James Version lakini wakashindwa kuelewa Kiingereza cha kale cha tafsiri hiyo. Mark alikumbuka kwamba bado alikuwa na Biblia na vitabu alivyopewa na Mashahidi miaka kadhaa iliyopita. Mark na Kathi waliisoma Biblia na kitabu Kweli Iongozayo Kwenye Uzima wa Milele na kitabu Is the Bible Really the Word of God? Walivutiwa sana na mambo waliyojifunza.
Mark asema hivi: “Nilivutiwa hasa niliposoma kwenye kitabu Kweli kuhusu kikundi cha Wakristo ambao hawakushiriki vita kamwe. Niliona kwamba hao ndio Wakristo wa kweli.” Muda mfupi baadaye, Mark na Kathi walirudi Houghton, Michigan, ili kutembelea jamaa ya Kathi—licha ya hatari ya kukamatwa. Walihudhuria mkutano wa Mashahidi huko wakiwa wamevalia kihuni na wakiwa na nywele ndefu. Walikubali funzo la Biblia na wakajifunza kwa mwezi mzima walipokuwa Michigan.
Baada ya kurudi kwenye Kisiwa cha Gabriola, walikutana na Shahidi mmoja barabarani huko Nanaimo, British Columbia, wakamwambia kwamba walitaka kujifunza Biblia. Siku hiyohiyo Mashahidi kadhaa walikuja kwa gari kupitia feri, na funzo la Biblia likaanzishwa. Miezi mitatu baadaye, Mark na Kathi walianza kuhubiri, kisha wote wawili wakabatizwa baada ya miezi mingine mitatu, Machi 10, 1974.
-
-
Wakutana kwa Njia ya Pekee Baada ya Miaka 30Amkeni!—2002 | Oktoba 22
-
-
Mark Aanza Utumishi wa Wakati Wote
Mwaka wa 1976, Mark pamoja na maelfu ya vijana wengine Wamarekani waliotorokea Kanada ili wasiandikishwe jeshini, walisamehewa na serikali ya Marekani. Yeye na mkewe, Kathi, walitamani pia kuishi maisha sahili ili watumie wakati mwingi zaidi katika utumishi. Kwa hiyo Mark alifanya kazi ya usoroveya kwa muda, na hivyo wakalipa madeni mengi waliyokuwa nayo kabla ya kubatizwa.
Mnamo mwaka wa 1978, Mark na Kathi walijitolea kushiriki ujenzi wa ofisi mpya ya tawi ambayo Mashahidi wa Kanada walikuwa wakipanga kujenga karibu na Toronto, Ontario. Walialikwa kwa sababu Mark alikuwa na ujuzi wa usoroveya. Walishiriki ujenzi wa ofisi huko Georgetown hadi kazi ilipokamilika mwezi wa Juni 1981. Baadaye, walirudi British Columbia na kwa miaka minne iliyofuata walishiriki ujenzi wa Jumba la Kusanyiko la Mashahidi wa Yehova huko. Ujenzi ulipokamilika, waliitwa tena kushiriki kazi ya upanuzi wa ofisi ya tawi ya Kanada.
Mwaka wa 1986, baada ya kukaa Georgetown kwa miezi kadhaa, Mark na Kathi walialikwa kuwa wafanyakazi wa wakati wote katika ofisi ya tawi ya Kanada. Wamekuwa wakifanya kazi huko tangu wakati huo na wameshiriki kazi ya ujenzi katika nchi nyingine nyingi. Kwa sababu ya ujuzi wake, Mark alianza kutumiwa kama soroveya wa majengo ya ofisi ya tawi na Majumba ya Kusanyiko ya Mashahidi wa Yehova katika Amerika ya Kusini na ya Kati na katika visiwa vya Karibea.
Kwa miaka mingi, Mark na Kathi walitumikia nchini Venezuela, Nikaragua, Haiti, Guyana, Barbados, Bahamas, Dominika, Marekani (Florida), na Jamhuri ya Dominika. Utumishi huo wa pekee wa wakati wote uliwakutanisha tena Mark na Dennis.
Wakutana Katika Jamhuri ya Dominika
Bila kujua, Mark na Dennis walishiriki kazi ya ujenzi katika Jamhuri ya Dominika. Siku moja walikutana ghafula katika ofisi ya tawi ya Mashahidi wa Yehova huko Santo Domingo. Hebu wazia furaha waliyokuwa nayo walipokutana tena. Miaka 33 ilikuwa imepita tangu walipoachana na walikuwa na mengi ya kuelezana. Walistaajabu walipokuwa wakisimulia mambo uliyosoma hapo juu. Lakini linalowastaajabisha zaidi—na vilevile wengine ambao wamewasimulia matukio hayo—ni jinsi ambavyo maisha yao yanavyofanana sana.
Wote waliishi maisha ya kihuni na kuhamia maeneo ya mashambani ili kuepuka maisha ya kisasa ya kutafuta mali na yenye mahangaiko mengi. Dennis alimwoa msichana anayeitwa Kathy; Mark alimwoa msichana anayeitwa Kathi. Wote wawili walikubali funzo la Biblia walipohudhuria mikutano ya Mashahidi wa Yehova kwa mara ya kwanza. Wote walibatizwa mwezi wa Machi 1974. Wote wakawa wafanyakazi kwenye ofisi ya tawi ya Mashahidi wa Yehova—Dennis nchini Marekani na Mark nchini Kanada. Wote wamejitahidi kuishi maisha sahili ili kufuatia miradi ya kiroho. (Mathayo 6:22) Wote walishiriki kazi ya ujenzi ya ulimwenguni pote na wamepewa migawo katika nchi nyingi. Hakuna yeyote kati yao aliyekuwa amekutana na rafiki wa zamani ambaye alikubali kweli za Biblia hadi walipokutana ghafula katika Jamhuri ya Dominika.
Je, Mark na Dennis wanaamini kwamba maisha yao yanafanana kwa sababu yaliamuliwa hivyo kimbele? La hasha. Kama Biblia inavyosema, wanatambua kwamba “wakati na tukio lisilotazamiwa [hutupata sote]”—wakati mwingine kwa njia za kushangaza sana. (Mhubiri 9:11, NW) Hata hivyo, wanatambua jambo jingine lililowakutanisha: jitihada yao kubwa ya kutafuta kusudi la maisha na upendo wao kwa Yehova Mungu.
Masimulizi ya maisha ya Dennis na Mark yanakazia pia baadhi ya mambo yanayowapata watu wote wanyofu wanaojifunza kweli ya Biblia. Dennis asema: “Maisha yangu na ya Mark yanaonyesha kwamba Yehova anajua hali za watu, naye huwavuta wanapokuwa na mwelekeo unaofaa.”—2 Mambo ya Nyakati 16:9; Yohana 6:44; Matendo 13:48.
Mark aongeza hivi: “Maisha yetu yametusaidia pia kutambua kwamba mtu anapojirekebisha kupatana na kanuni za Yehova, anapojiweka wakfu, na kuwa tayari kutumiwa, Yehova anaweza kutumia vipawa na uwezo wake ili kuendeleza ibada ya kweli kwa faida ya watu wake.”—Waefeso 4:8.
Maisha yao yanaonyesha pia kwamba Yehova Mungu huwabariki watu wake wanaomtumikia kwa nafsi yote. Bila shaka Dennis na Mark wamebarikiwa. Dennis anasema hivi: “Ni pendeleo kushughulikia masilahi ya Ufalme katika utumishi wa pekee wa wakati wote. Tumefurahia kutiana moyo tunapofanya kazi pamoja na ndugu na dada zetu Wakristo kutoka sehemu zote za ulimwengu.”
Mark aongezea hivi: “Hapana shaka kwamba Yehova hubariki wale wanaotanguliza Ufalme. Mimi naona ni pendeleo la pekee sana kuwa mshiriki wa familia ya ofisi ya tawi ya Kanada na kushiriki kazi ya ujenzi ya ulimwenguni pote.”
Je, walikutana kwa njia ya pekee? Naam, kwa sababu kama Mark anavyosema: “Jambo muhimu lililofanya kukutana kwetu kusisimue sana ni kuwa sote wawili tumekuja kumjua, kumpenda, na kumtumikia Mungu wa pekee, Yehova.”
-
-
Wakutana kwa Njia ya Pekee Baada ya Miaka 30Amkeni!—2002 | Oktoba 22
-
-
[Picha katika ukurasa wa 21]
Mark, mwaka wa 1964
-
-
Wakutana kwa Njia ya Pekee Baada ya Miaka 30Amkeni!—2002 | Oktoba 22
-
-
[Picha katika ukurasa wa 23]
Mark akiwa Ontario, mwaka wa 1971
[Picha katika ukurasa wa 24]
Dennis na Mark, pamoja na wake zao, punde tu baada ya kukutana kwa ghafula mwaka wa 2001
-