Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Uvutio wa Vitabu Vidogo Sana
    Amkeni!—1998 | Aprili 22
    • Biblia Gumba

      Biblia Gumba si lazima ziwe Biblia nzima. Nyingine ni “Agano Jipya tu.” Nyingine ni muhtasari wa hadithi za Biblia au huwa na historia nzima ya Biblia ikiwa imefupishwa kufikia karibu maneno 7,000, na zilibuniwa hasa kwa ajili ya kusomwa na watoto. Zina vichwa kama vile The Bible in Miniature, The History of the Holy Bible, na The Child’s Bible.

      Biblia gumba ilipataje jina lake? Ufafanuzi ulio wazi ni kwamba Biblia hiyo ni kubwa kidogo tu zaidi ya ncha ya kidole gumba cha mwanadamu. Na bado kitabu Three Centuries of Thumb Bibles hudokeza kwamba maneno hayo huenda yalitungwa kufuatia ziara ya Mmarekani mmoja mfupi sana Charles Stratton huko Uingereza, anayejulikana vyema kuwa Jenerali Tom Thumb. Jambo linalounga mkono dai hili ni uhakika wa kwamba Tom Thumb alizuru Uingereza katika mwaka wa 1844 na maneno “Biblia gumba” yaonekana kuwa yalitumiwa kwa mara ya kwanza katika London katika mwaka wa 1849.

      Mabuku ya Maandiko Yasiyo ya Kawaida

      Tunu iliyoongezewa kwenye ulimwengu wa Biblia ndogo ni The Finger New Testament, iliyochapishwa karibu mwanzoni mwa karne ya 20. Ina upana wa sentimeta tatu tu na urefu wa sentimeta tisa—urefu wa kidole—kwa hiyo, ikapewa jina hilo. Hata hivyo, kwa kuwa ina urefu unaozidi milimeta 76, tukisema kwa kweli, si kitabu kidogo sana, ijapokuwa kwa kawaida huainishwa pamoja na Biblia kama hizo. Herufi zake ndogo sana za chapa, zilizotumiwa katika buku hili ndogo ni dhahiri kabisa na huweza kusomwa na wengi bila kuzikuza.

      Kielelezo kimoja kisicho cha kawaida kina kichwa The Illustrated Bible, chenye mashairi yaliyo na kichwa Railway to Heaven. Kiliendelea kuchapishwa kwa zaidi ya miaka 50 wakati wa siku za mapema za ujenzi wa reli za Uingereza. Mwandishi akitumia reli kujifaidi aliandika shairi la kurasa mbili, lenye kichwa “Kuwaelekeza Kwenye Njia Nyingine.” Njia hiyo nyingine inatambulishwa kuwa “Yesu Kristo, Mwana wa Yehova.” Shairi hilo lamalizia: “Mwana wangu, asema Mungu, elekeza moyo wako kwangu. Fanya hima—ama sivyo utaachwa na gari moshi.”

  • Uvutio wa Vitabu Vidogo Sana
    Amkeni!—1998 | Aprili 22
    • Biblia ya “Agano Jipya” iliyo ndogo zaidi kupata kutolewa ilikuwa ya David Bryce, wa Glasgow, Scotland, katika mwaka wa 1895. Ina urefu wa sentimeta 1.9 kwa upana wa sentimeta 1.6 na unene wa sentimeta 0.8! Iliwezekanaje kuichapisha? “Ilichapishwa vizuri sana kwa kutumia njia ya kupunguzia ukubwa wa chapa kwa mashine,” aeleza Louis Bondy katika Miniature Books. Upigaji wa picha ukiwa umeanzishwa tu miaka mia moja iliyopita, hili lilikuwa fanikio kubwa sana.

      Pia David Bryce alichapisha idadi kadhaa za Biblia Gumba akitumia njia hiihii. Kwa wale walio na tatizo la kusoma nakala ndogo sana, kila Biblia ina kiookuzi kidogo kilichotiwa ndani ya jalada la kuunganisha. Wakitumia msaada huu, kusoma kwawezekana kwa wale wanaostahimili.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki