-
Mahali Ambapo Mabara Sita HuunganaAmkeni!—2005 | Februari 22
-
-
Emu ni ndege mkubwa asiyeweza kuruka kutoka Australia. Yeye ndiye ndege wa pili kwa ukubwa, kwani mbuni tu ndiye anayemzidi. Emu fulani huwa na kimo cha meta 1.8, nao huwa na uzani wa kilo 59. Ijapokuwa ua limewatenganisha na wanyama, wana nafasi kubwa ya kukimbia huku na huku.
Emu ni ndege wa pekee kwani vifaranga wake huitikia sauti ya emu wa kiume wanapokuwa ndani ya mayai. Kwa mfano, inasemekana kwamba sauti ya emu wa kiume inapochezwa kabla tu ya mayai kuanguliwa, vifaranga walio ndani ya mayai husongasonga na kufanya mayai yatikisike. Hata hivyo, vifaranga wanapokuwa ndani ya mayai hawaitikii sauti ya emu wa kike. Kwa nini?
Ijapokuwa emu wa kike hutaga mayai, emu wa kiume ndiye huyalalia. Yeye huyatunza kwa siku 50 hivi hadi yanapoanguliwa, kisha huwatunza vifaranga. Kwa hiyo, hata kabla ya mayai kuanguliwa, vifaranga hutambua yule anayewatunza. Hayo si mayai ya kawaida kwani yana rangi ya kijani kibichi, ni makubwa sana, na yana uzani wa gramu 700 hivi!
-
-
Mahali Ambapo Mabara Sita HuunganaAmkeni!—2005 | Februari 22
-
-
[Picha katika ukurasa wa 15]
Emu
-