-
Brolga, Kasowari, Emu, na Jabiru—Baadhi ya Ndege Wenye Kutazamisha wa AustraliaAmkeni!—1996 | Novemba 8
-
-
Na mwenye kupita hapo karibu, mrefu na mwembamba, jabiru ni kielelezo cha adhama na usawaziko wa kindege.
-
-
Brolga, Kasowari, Emu, na Jabiru—Baadhi ya Ndege Wenye Kutazamisha wa AustraliaAmkeni!—1996 | Novemba 8
-
-
Jabiru—Koikoi Pekee wa Australia
Akiwa ndege wa mabwawa, jabiru, au koikoi mwenye shingo nyeusi, huzuru mara nyingi pwani zenye joto na unyevu za kaskazini na mashariki mwa Australia. (Jabiru wa Amerika Kusini ni spishi tofauti ya koikoi.) Akiwa mwembamba, mwenye kimo cha sentimeta 130, mwenye rangi yenye kupendeza, jabiru huonekana kwa urahisi miongoni mwa mamiriadi ya ndege wengineo wa mabwawa. Atembeapo katika maji yasiyo na kina kirefu, yeye atapiga kwa ghafula mdomo wake mrefu na wenye nguvu kuingia majini kwa nguvu nyingi sana hivi kwamba atahitaji kutikisa mabawa yake yafunguke kidogo ili kukabiliana na kani hiyo.
Na mabawa hayo ni yenye uweza kama nini! Akipanua mabawa yake kwa meta mbili kuanzia ncha moja hadi nyingine, akiwa na manyoya makuu yakiwa yameenea kama vidole, jabiru hupuruka kwa kuelea polepole kimviringo hadi aonekana akiwa kama kisalaba kidogo angani. Kwa kweli, jabiru akiwa hewani, akiwa na mabawa yake marefu, shingo ndefu na miguu mirefu akitokeza umbo jeusi dhidi ya jua kubwa jekundu la kiikweta lenye kutua, ni mfano unaothaminiwa sana wa mabwawa ya kaskazini mwa Australia.
-