Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Brolga, Kasowari, Emu, na Jabiru—Baadhi ya Ndege Wenye Kutazamisha wa Australia
    Amkeni!—1996 | Novemba 8
    • AKIWA na kucha zenye kutisha, kasowari asiyeweza kupuruka, mwenye kufafanuliwa kuwa ndege hatari kuliko wote ulimwenguni, aweza kuruka, kupiga teke, na kurarua, kwa nguvu zenye kushangaza.

  • Brolga, Kasowari, Emu, na Jabiru—Baadhi ya Ndege Wenye Kutazamisha wa Australia
    Amkeni!—1996 | Novemba 8
    • Kasowari Mwenye Rangi Nyingi —Mfadhili wa Msitu wa Mvua

      Akiwa na uzani wa kilogramu kati ya 30 na 60, kasowari wa kusini, au mwenye dehedehe mbili, wa misitu ya mvua yenye kusitawi sana ya kaskazini-mashariki mwa Australia na wa New Guinea ni ndege mwenye kuvutia lakini mpweke. Akiwa mwenye kimo cha meta mbili hivi, wa kike ni mkubwa kuliko wa kiume na—jambo lisilo kawaida kwa ndege—ni mwenye rangi nyingi kidogo kuliko wa kiume, ambaye mbali na msimu wa kujamiiana kwa hekima hukaa mbali naye. Baada ya kujamiiana, jike hutaga kikundi cha mayai yenye rangi ya kijani chenye kung’aa, lakini kisha huenda zake, akimwacha dume kuyaatamia na kutunza makinda. Kisha ajamiiana na madume wengine na kuacha kila mmoja wao akiwa na kikundi cha mayai ya kutunza!

      Hata hivyo, kukatwa kwa misitu kunawadhuru kasowari. Katika jaribio la kuongeza idadi yao, Hifadhi ya Billabong karibu na Townsville, Queensland, imeanzisha programu ya uzalishaji wa utekwani inayonuia kuwaachilia ndege warudi porini wanapokuwa wenye umri wa kutosha. Ingawa hula wanyama na mimea, kasowari hasa hula matunda, ambayo huyameza yakiwa mazima. Hivyo, mbegu za zaidi ya spishi mia za mimea husafiri bila kumeng’enywa kupitia utumbo na kusambazwa sana kotekote msituni katika mbolea yenye lishe. Hilo, wasema wataalamu wa hifadhi hiyo, laweza kumfanya kasowari awe spishi yenye kutegemewa, katika maana ya kwamba akitoweka spishi nyingi za mimea zitatoweka. Lakini je, ndege huyu ni hatari kwa wanadamu?

      Ni hatari kwa watu wapumbavu tu ambao hukaribia sana. Kihalisi, wanadamu ndio tisho kubwa zaidi kwa kasowari kuliko vile yeye amepata kuwa tisho kwao. Katika vivuli vyenye giza-giza vya msitu wa mvua, ndege huyo atanguruma kwa kina kutoka kooni ili kukuonya kwamba yuko karibu. Kubali onyo; usiende karibu zaidi. Yaelekea sana, atatoka kwa kishindo kupitia kichaka, akitumia dirii yake ngumu ili kulinda kichwa chake. Lakini anapozuiwa kwenye pembe fulani, au kuumizwa au anapolinda mtoto wake, aweza kushambulia ukisonga karibu sana.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki