-
Mbuga ya Kipekee ya Wanyama wa MediteraniaAmkeni!—2002 | Mei 22
-
-
Ndege wa Biblia
Ingawa mbuga hiyo ni ndogo, hiyo ni makao ya kanu, mbawala mwekundu, nguruwe-mwitu, na simba-mangu wa Hispania ambaye haonekani sana na ambaye ni mmoja wa wanyama walio katika hatari kubwa ya kutoweka huko Ulaya. Kwa sababu wanyama walio wengi hutembea usiku, ni rahisi kwa mgeni anayezuru mchana kuona tu ndege walao nyama wenye kuvutia ambao wanapatikana kwa wingi kuliko kuwaona wanyama hao. Wengi wa ndege hao pia walipatikana kwa wingi nyakati za Biblia.
Katikati ya karne ya 19, mwanasayansi mmoja kwa jina H. B. Tristram aliwaona tumbusi aina ya griffon wenye madoadoa wakiruka angani aliposafiri huko Palestina. Ndege hao huonekana pia huko Monfragüe, ambapo ndege 800 wamejenga viota katika miamba inayoelekea mto wa Targus na Tiétar. Wakati wa jioni, tumbusi wengi huruka juu wakizunguka viota vyao vya pamoja, huku maumbo yao makubwa meusi yakionekana kama madoa yanayotapakaa kotekote angani.b
Korongo weupe wanaojenga viota katika nyumba nzee za sehemu nyingi za Ulaya, bado wanajenga viota katika mialoni ya Monfragüe ambapo wanasitawi. (Zaburi 104:17) Pamoja na korongo, ndege wengine wanaopaa bila kuchoka katika ukanda wenye joto ni tai-mfalme na tai-dhahabu ambao ‘huangalia toka mbali’ wakitafuta windo lao.—Ayubu 39:27-29.
Wakati wa kiangazi mwewe wekundu huongezeka, ambao ni wepesi na wengi kuliko tai. Pia, tai weusi ambao wana macho makali huruka wakitafuta daima kunasa samaki katika maji ya mito iliyomo katika hifadhi hiyo.—Ayubu 28:7
Aina nyingine za ndege walao nyama, kama bundi-tai na bundi babewatoto, huanza kuruka angani wakati wa usiku. Bundi tai hutengeneza kiota katika majabali yaliyo mbali ya Monfragüe, sawa tu na mahali penye magofu ya Babiloni ya kale ambapo nabii Isaya alitabiri kwamba bundi angekaa.—Isaya 13:21
-
-
Mbuga ya Kipekee ya Wanyama wa MediteraniaAmkeni!—2002 | Mei 22
-
-
[Picha katika ukurasa wa 18]
Tumbusi mweusi
[Picha katika ukurasa wa 18]
Bundi-mwewe
[Picha katika ukurasa wa 18]
Tai-dhahabu
[Hisani]
Fotos: Cortesía de GREFA
-