Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kuhifadhi Joto Katika Theluji
    Amkeni!—2008 | Februari
    • Bundi pia huwinda. Bundi mkubwa wa rangi ya kijivu ana uwezo mkubwa wa kusikia hivi kwamba anaweza kumfuata panyabuku anayetembea chini ya theluji ikiwa theluji hiyo si yenye kina kirefu. Bundi anapomwona mnyama anayetaka, anaruka na kuingia ndani ya theluji na kumbeba akitumia kucha zake.

  • Kuhifadhi Joto Katika Theluji
    Amkeni!—2008 | Februari
    • Kuingia Ndani ya Theluji!

      Ndege kadhaa hutumia uwezo wa theluji wa kuzuia baridi isipenye kwa kupumzika wakati wa mchana au kulala wakati wa usiku chini ya theluji. Ndege hao wanatia ndani hazel hen, kwale weusi, na ptarmigan, pia ndege wadogo zaidi kama vile linnet, aina fulani ya shorewanda, na shore. Ikiwa theluji ina kina kirefu na ni nyororo, ndege fulani huingia ndani ya theluji, kama vile tu ndege wa baharini wanavyopiga mbizi majini. Mbinu hiyo inawasaidia wasiache alama zitakazoonekana au kunuswa na wanyama wanaowinda.

      Baada ya kuingia ndani ya theluji, ndege hao wanachimba shimo lenye upana wa sentimita 60 hivi linaloitwa kieppi katika Kifini. Upepo unaovuma usiku unafanya isiwe rahisi kutambua kwamba kuna viumbe chini ya theluji. Watu wanaotembea wanapofika karibu sana, ndege hao wanawasikia kwa sababu ya kelele ya kutembea kwao. Wanaporuka ghafula na kutifua theluji huku wakipiga mabawa yao wanaweza kumshtua sana mtu ambaye hakuwatarajia.

  • Kuhifadhi Joto Katika Theluji
    Amkeni!—2008 | Februari
    • Vivyo hivyo, ptarmigan hubadilisha manyoya yake yenye madoadoa ya majira ya kiangazi na kupata manyoya meupe kabisa. Pia, kucha zao ambazo huwa hazina manyoya mengi wakati wa kiangazi, zinakuwa na manyoya mengi na hivyo anakuwa ni kama amevaa viatu vya theluji.

  • Kuhifadhi Joto Katika Theluji
    Amkeni!—2008 | Februari
    • Je, umewahi kujiuliza ni kwa nini ndege, wengi wao wanaotembea kwenye theluji au barafu bila viatu hawapati madhara? Kwa sababu wana mfumo wa kuongeza joto miguuni. Mfumo huo wa ajabu unafanya damu yenye joto kutoka kwa moyo iende miguuni na kupasha joto damu baridi inayotoka miguuni.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki