-
Kufungua Kufuli ya Siri TakatifuUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
16. (a) Viongozi wa Jumuiya ya Wakristo walionyesha uchukivu wa pekee kwa nani? (b) Ni jambo gani lililotukia katika Jumuiya ya Wakristo katika kile kipindi cha zile Enzi za Katikati? (c) Je! ule uasi au Mapinduzi Makuu ya Kiprotestanti, yalibadili njia za uasi-imani za Jumuiya ya Wakristo?
16 Huku wakidai kuwa wachungaji wa kundi la Mungu, viongozi wa Jumuiya ya Wakristo, wa kidini na wa kiserikali, walionyesha uchukivu wa pekee kwa yeyote aliyejaribu kutia moyo usomaji wa Biblia au yeyote aliyefichua mazoea yao yasiyo ya kimaandiko. John Hus na mtafsiri Biblia William Tyndale, walinyanyaswa na wakauawa kwa sababu ya imani yao. Katika kile kipindi chenye kutiwa giza cha Enzi za Katikati, utawala wa wenye kuasi imani ulifikia upeo wao kwa lile Baraza la Kuhukumia Wazushi wa Kidini lenye ukatili mwingi la Kikatoliki. Watu wowote waliopinga mafundisho au mamlaka ya kanisa walikandamizwa bila rehema, na maelfu yasiyohesabika ya wale walioitwa eti wazushi wa kidini waliteswa-teswa mpaka kifo au wakachomwa penye nguzo. Hivyo Shetani alijitahidi kuhakikisha kwamba mbegu yoyote ya kweli ya tengenezo la Yehova lililo mfano wa mwanamke ingepondwa-pondwa kwa haraka sana. Wakati ule uasi au Mapinduzi Makuu ya Kiprotestanti yalipotukia (kuanzia 1517 na kuendelea), makanisa mengi ya Kiprotestanti yalidhihirisha roho ile ile ya kutovumilia. Hayo vilevile yakawa yenye hatia ya damu kwa kuwaua kwa sababu ya imani yao wale wote waliojaribu kuwa washikamanifu kwa Mungu na Kristo. Kweli kweli, “damu ya watakatifu” ilimwagwa kwa wingi sana!—Ufunuo 16:6; linga Mathayo 23:33-36.
-
-
Kufungua Kufuli ya Siri TakatifuUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Yesu alipoanza ukaguzi wake katika 1918, hapana shaka viongozi wa kidini wa Jumuiya ya Wakristo walipokea hukumu mbaya. Hawakuwa wameanzisha tu mnyanyaso mbaya dhidi ya watu wa Mungu bali pia walijiletea hatia ya damu kwa kuunga mkono yale mataifa yaliyokuwa yakipigana katika kipindi cha ile vita ya ulimwengu ya kwanza. (Ufunuo 18:21, 24) Kisha hao viongozi wa kidini wakaweka tumaini lao katika ule Ushirika wa Mataifa uliofanyizwa na mwanadamu. Pamoja na milki yote nzima ya dini bandia ya ulimwengu, Jumuiya ya Wakristo ilikuwa imeanguka kabisa kutoka kibali cha Mungu kufikia 1919.
-
-
Kufungua Kufuli ya Siri TakatifuUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
[Picha katika ukurasa wa 31]
Dini ya Jumuiya ya Wakristo ilijiletea hatia ya damu kubwa kwa kunyanyasa na kuua wale waliotafsiri, wakasoma, au hata wakawa na Biblia
-