Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Twatambuliwa kwa Mwenendo Wetu
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • Katika Puerto Riko katika Novemba 1976, Ana Paz de Rosario mwenye umri wa miaka 45, alikubali upasuaji na utibabu uliohitajiwa lakini akaomba kwamba kwa sababu ya imani zake za kidini, damu isitumiwe. Hata hivyo, wakiwa na amri ya mahakama, polisi watano na wauguzi watatu walikwenda katika chumba chake cha hospitali baada ya usiku kati, wakamfunga kwenye kitanda, na kumtia damu mishipani kwa nguvu, kinyume cha mapenzi yake na yale ya mume na watoto wake. Alipatwa na mshtuko, akafa.

  • Twatambuliwa kwa Mwenendo Wetu
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • Katika Italia, katika 1982, mume na mke waliokuwa wametafuta kwa upendo msaada wa kitiba katika nchi nne kwa ajili ya binti yao aliyekuwa na ugonjwa usioponyeka walihukumiwa miaka 14 gerezani kwa shtaka la uuaji-kimakusudi baada ya msichana wao kufa alipokuwa akitiwa damu mishipani kwa amri ya mahakama.

      Mara nyingi, kuhusiana na majaribio ya kutia damu mishipani kwa nguvu katika watoto wa Mashahidi wa Yehova, uhasama mwingi wa umma umechochewa na vyombo vya habari. Katika visa fulani, hata bila kusikilizwa na mahakama ili wazazi waeleze, mahakimu wameamuru kwamba watoto wao watiwe damu mishipani. Hata hivyo, katika visa zaidi ya 40 katika Kanada, watoto waliotiwa damu mishipani walirudishwa kwa wazazi wao wakiwa wamekufa.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki