Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Yehova Mungu Awarehemu Mabaki
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 13. Isaya afafanuaje mabaki ambao Yehova angewarehemu, kama ilivyorekodiwa katika Isaya 4:3?

      13 Tayari tumefahamishwa juu ya mabaki ambao Yehova angerehemu, lakini sasa Isaya awafafanua kinaganaga. Aandika: “Itakuwa ya kwamba yeye aliyebaki katika Sayuni, na yeye aliyeachwa ndani ya Yerusalemu, ataitwa mtakatifu; yaani, kila mmoja aliyeandikwa miongoni mwa hao walio hai ndani ya Yerusalemu.”—Isaya 4:3.

  • Yehova Mungu Awarehemu Mabaki
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 15. (a) Usemi ‘walioandikwa kwa ajili ya uhai ndani ya Yerusalemu’ watukumbusha desturi gani ya Wayahudi? (b) Maneno ya Isaya yadokeza onyo gani linalofaa kuzingatiwa?

      15 Je, mabaki waaminifu hao watadumu humo? “[Wata]andikwa miongoni mwa hao walio hai [“wataandikwa kwa ajili ya uhai,” NW] ndani ya Yerusalemu,” Isaya aahidi. Hilo latukumbusha desturi ya Wayahudi ya kuweka rejesta za familia na makabila ya Israeli kwa makini. (Nehemia 7:5) Kuandikwa katika rejesta kulimaanisha kwamba mtu yu hai, kwa sababu alipokufa, jina lake liliondolewa. Katika sehemu nyinginezo za Biblia, twasoma juu ya rejesta ya kitamathali, au kitabu, chenye majina ya wale ambao Yehova huwapa thawabu ya uhai. Ijapokuwa kuna masharti ya kuandikwa majina katika kitabu hicho, kwa kuwa Yehova aweza ‘kufuta’ majina. (Kutoka 32:32, 33; Zaburi 69:28) Basi, maneno ya Isaya yadokeza onyo linalofaa kuzingatiwa—wenye kurudi waweza kuendelea kuishi katika nchi yao iliyorudishwa maadamu wadumisha utakatifu machoni pa Mungu.

  • Yehova Mungu Awarehemu Mabaki
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 17. Yehova huandika majina ya nani katika “kitabu [chake] cha uhai,” nasi twapaswa kuazimia kufanya nini?

      17 Kumbuka kwamba Yehova aliwaona wale waliokuwa watakatifu nchini Israeli naye ‘akayaandika majina yao kwa ajili ya uhai.’ Leo pia, Yehova huona jitihada zetu za kuwa safi katika akili na mwili ‘tutoapo miili yetu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, yenye kukubalika kwa Mungu.’ (Waroma 12:1) Naye Mungu huwarekodi wote wanaofuata mwendo huo wa maisha katika “kitabu [chake] cha uhai”—rekodi ya kitamathali yenye majina ya wale wanaotarajia kupata uhai udumuo milele, huko mbinguni au hapa duniani. (Wafilipi 4:3; Malaki 3:16) Basi, na tufanye kila tuwezalo ili kudumisha utakatifu machoni pa Mungu, ndipo twaweza kudumisha majina yetu katika “kitabu” hicho chenye thamani.—Ufunuo 3:5.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki