-
Hatua Muhimu Katika Kutokeza Biblia za Lugha za KiafrikaMnara wa Mlinzi—2007 | Januari 15
-
-
Hatua nyingine muhimu ya kutokeza Biblia katika lugha za Kiafrika ilifikiwa mnamo Agosti (Mwezi wa 8) 2005. Mwezi huo, nakala zaidi ya 76,000 za Tafsiri ya Ulimwengu Mpya katika lugha mbalimbali zinazozungumzwa barani Afrika zilichapishwa na kutiwa jalada katika ofisi ya tawi ya Mashahidi wa Yehova nchini Afrika Kusini. Nakala hizo zilitia ndani Biblia 30,000 za lugha ya Kishona. Biblia hiyo ya Kishona ilitolewa kwenye Makusanyiko ya Mashahidi wa Yehova ya “Utii wa Kimungu” nchini Zimbabwe.
Katika mwezi huo wa pekee, watu waliotembelea ofisi ya tawi ya Afrika Kusini walifurahia sana kuona Biblia mpya za lugha za Kiafrika zikichapishwa. “Nilifurahi sana na kusisimka kupata pendeleo la kushiriki katika kazi ya kutokeza Tafsiri ya Ulimwengu Mpya katika Kishona na katika lugha nyingine za Kiafrika,” anasema Nhlanhla, mwanabetheli anayefanya kazi ya kutia vitabu jalada. Bila shaka, hayo ndiyo maoni ya familia nzima ya Betheli ya Afrika Kusini.
Biblia mpya zitawafikia watu barani Afrika haraka zaidi na kwa gharama ya chini kuliko ilivyokuwa zilipokuwa zikichapishiwa katika nchi za ng’ambo na kusafirishwa kutoka huko. La muhimu zaidi ni kwamba, sasa Waafrika wana tafsiri sahihi inayotumia jina takatifu la Mtungaji mkuu wa Biblia, Yehova Mungu.
-
-
Hatua Muhimu Katika Kutokeza Biblia za Lugha za KiafrikaMnara wa Mlinzi—2007 | Januari 15
-
-
[Picha katika ukurasa wa 13]
Wageni kutoka Swaziland wanatazama Biblia mpya zinazochapishwa katika ofisi ya tawi ya Afrika Kusini
-