-
Matatizo ya Kutafsiri Biblia ya KiitalianoMnara wa Mlinzi—2005 | Desemba 15
-
-
Kitabu kimoja (Enciclopedia Cattolica) kinasema hivi: “Sikuzote Kanisa limefaulu kudhibiti vitabu, lakini kabla ya uchapaji kuvumbuliwa, halikuona uhitaji wa kuwa na orodha ya vitabu vilivyokatazwa kwa sababu vitabu vilivyoonwa kuwa hatari viliteketezwa.”
-
-
Matatizo ya Kutafsiri Biblia ya KiitalianoMnara wa Mlinzi—2005 | Desemba 15
-
-
Mwaka wa 1559, Papa Paul wa Nne, alichapisha orodha ya kwanza ya vitabu vilivyokatazwa, yaani, orodha ya vitabu ambavyo Wakatoliki walikatazwa kusoma, kuuza, kutafsiri, au kuwa navyo. Vitabu hivyo vilionwa kuwa viovu na hatari kwa imani na maadili. Orodha hiyo ilipiga marufuku kusoma Biblia zilizotafsiriwa katika lugha za kienyeji, kutia ndani tafsiri ya Brucioli. Wale waliokiuka sheria hizo walifukuzwa kanisani. Orodha ya mwaka wa 1596 ilikuwa na sheria kali hata zaidi. Ilipiga marufuku kutafsiri au kuchapisha Biblia katika lugha za kienyeji. Biblia hizo zilipaswa kuharibiwa.
-
-
Matatizo ya Kutafsiri Biblia ya KiitalianoMnara wa Mlinzi—2005 | Desemba 15
-
-
[Picha katika ukurasa wa 15]
Orodha ya vitabu vilivyokatazwa ilisema kwamba tafsiri za Biblia katika lugha za kienyeji ni hatari
-