-
Matukio Muhimu ya mwaka uliopita2009 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
Ofisi ya tawi iliyopanuliwa nchini Nigeria, iliwekwa wakfu Juni 7, 2008 jijini Lagos, umbali wa kilomita 360 kusini-magharibi ya Betheli ya Igieduma. Ofisi ya Lagos ina jengo la makao lenye vyumba 24, bohari, na jengo la ofisi. Mambo mengi yanayohusu ofisi ya tawi yanashughulikiwa huko Lagos, mji mkuu wa biashara wa nchi hiyo. Wanabetheli wanaochukua vitu kutoka bandarini na kununua vitu vinavyohitajiwa kwenye ofisi ya tawi, na pia ndugu wanaowasili na kuondoka kwenye uwanja wa ndege, wanalala katika ofisi hiyo. Ofisi ya Lagos pia inatumika kwa ajili Shule ya Mazoezi ya Kihuduma mpaka upanuzi wa ofisi ya tawi ya Igieduma ukamilike. Kwa kweli, Yehova anabariki kazi ya kuhubiri barani Afrika, kama anavyofanya duniani kote.
-
-
Matukio Muhimu ya mwaka uliopita2009 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
[Picha katika ukurasa wa 29]
Jengo jipya la makao jijini Lagos, Nigeria
-