-
Norway2012 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
KUNYANG’ANYWA VITABU, KUKAMATWA, NA KISHA MARUFUKU
Matatizo yalikuwa njiani. Kwa mara nyingine tena, polisi wa Ujerumani walikuja kwenye ofisi ya tawi, wakaitisha machapisho na kumhoji Ndugu Öman. Mwishoni mwa 1940, polisi hao waliwanyang’anya akina ndugu kitabu Enemies, kwa sababu ya maelezo yake kuhusu utawala wa Kifashisti na wa Wanazi.
-
-
Norway2012 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
Kisha, Wanazi wakaja ofisini na kuchukua akiba yote ya vijitabu viwili, Fascism or Freedom na Government and Peace.
-
-
Norway2012 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
Mnamo Julai 1941, Gestapo walianza jitihada za kusimamisha kazi ya kuhubiri kotekote nchini Norway. Polisi watano Wajerumani walikuja Betheli, wakachukua machapisho yaliyobaki na kuwapeleka Wanabetheli wote kwenye makao makuu ya polisi ili kuwahoji. Ndugu Öman alipaswa kuripoti kwa polisi kila siku, na alifanya hivyo kwa majuma 12.
-