-
Matukio Muhimu ya Mwaka Uliopita2008 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
Rwanda
Baada ya miaka 30 yenye msukosuko, kutia ndani kupigwa marufuku na vita vya wenyewe kwa wenyewe, ndugu na dada nchini Rwanda walifurahi kuwa na ndugu Guy Pierce kwenye kuwekwa wakfu kwa ofisi mpya maridadi ya tawi ambayo imejengwa katika bustani zenye kupendeza.
Licha ya matukio yenye kusikitisha ya mauaji ya kikabila, ambayo yalisababisha ndugu kadhaa kuuawa, kazi ya Yehova imeendelea kunawiri katika nchi hii inayojulikana kama Nchi ya Milima Elfu Moja. Watu 553 ambao walifurahia programu ya wakfu Jumamosi, Desemba 2, 2006, walitia ndani wajumbe 112 kutoka nchi 15.
-