-
Uganda2010 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
Mwaka wa 1995 Halmashauri ya Nchi iliwekwa rasmi itumikie chini ya ofisi ya tawi ya Kenya. Mojawapo ya makao ya wamishonari mjini Kampala yakawa makao ya wajitoleaji nane wa wakati wote, kutia ndani kikundi cha watafsiri wa Kiganda. Septemba 2003, Uganda ikawa ofisi ya tawi.
-
-
Uganda2010 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
Mwaka wa 2001, Baraza Linaloongoza lilitoa kibali uwanja wa ekari 10 ununuliwe kwa ajili ya ujenzi wa ofisi mpya ya tawi, nje kidogo ya mji wa Kampala, karibu na Ziwa Victoria.
Mwanzoni, kampuni iliyofaa zaidi kufanya ujenzi huo haikukubali ombi letu kwa kuwa ilikuwa na miradi mingine mingi ya ujenzi wakati huo. Lakini ajabu ni kwamba, bila kutazamia, ilibadili nia na kwa kushangaza, ikatoa makadirio bora zaidi ya gharama za ujenzi wa ofisi mpya ya tawi. Inaonekana kwamba walipoteza kandarasi kubwa ghafula, na hivyo wakalazimika kukubali kujenga ofisi ya tawi haraka iwezekanavyo.
Januari 2006, familia ya Betheli ilifurahi kuhamia makao yao mapya yenye kupendeza, ya orofa mbili zenye vyumba 32. Mbali na makao, kuna jengo la ofisi mbalimbali, jumba kubwa la kulia, jiko, na dobi. Pia kuna mfumo wa maji-taka unaopatana na kanuni za kimazingira, bohari kwa ajili ya idara ya upakizi na usafirishaji, na majengo yenye karakana za udumishaji, uhifadhi wa maji, na mitambo ya umeme. “Sasa tuko paradiso,” akasema ndugu mmoja kwa furaha tele, “uzima wa milele tu ndio tunakosa!” Hotuba ya kuweka wakfu ilitolewa Jumamosi, Januari 20, 2007, na Ndugu Anthony Morris wa Baraza Linaloongoza.
-
-
Uganda2010 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
[Picha katika ukurasa wa 124]
Ofisi ya Tawi ya Uganda
-
-
Uganda2010 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
majengo ya ofisi (chini) na makao (kulia)
-