Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Badala ya Dhahabu, Nilipata Almasi”
    Mnara wa Mlinzi—1997 | Machi 1
    • Katika mwaka wa 1945, nilialikwa kutumikia kwenye ofisi ya tawi ya Mashahidi wa Yehova katika Athene. Wakati huo, Betheli, neno limaanishalo “Nyumba ya Mungu,” ilikuwa katika nyumba ya kukodi kwenye Lombardou Street. Ofisi zilikuwa kwenye orofa ya kwanza, na mahali pa matbaa palikuwa katika chumba cha chini. Mahali hapo palikuwa na matbaa ndogo na mashine ya kukatia karatasi. Mwanzoni wafanyakazi kwenye mahali pa matbaa walikuwa watu wawili tu, lakini upesi wajitoleaji wengine walioishi nje ya Betheli walianza kuja kusaidia na kazi.

      Uwasiliano pamoja na makao makuu ya Watch Tower Society katika Brooklyn, New York, ulianzishwa tena katika mwaka wa 1945, na mwaka huo tukaanza tena kuchapa Mnara wa Mlinzi kwa ukawaida katika Ugiriki. Kisha, katika mwaka wa 1947, tulihamisha ofisi yetu ya tawi hadi 16 Tenedou Street, lakini mahali pa matbaa pakabaki Lombardou Street. Baadaye hapo mahali pa matbaa palihamishwa kutoka Lombardou Street hadi kiwanda cha Shahidi mmoja kilichokuwa umbali wa kilometa tano hivi. Kwa hiyo kwa kipindi fulani tulikuwa tukisafiri kwenda na kurudi kati ya mahali patatu.

      Nakumbuka nikiondoka makao yetu kwenye Tenedou Street asubuhi sana na kusafiri kwenda kwenye mahali pa matbaa. Baada ya kufanya kazi hapo hadi saa saba alasiri, nilienda Lombardou Street ambako karatasi tulizokuwa tumechapa zilipelekwa. Huko zilikunjwa kuwa magazeti, zikashonwa na kukatwa kwa mkono. Baadaye tulipeleka magazeti yaliyokamilika hadi kwenye ofisi ya posta, tukayabeba hadi orofa ya tatu, tukawasaidia wafanyakazi kuzitenganisha, na kuweka stampu juu ya bahasha ili kuzituma.

      Kufikia mwaka wa 1954 idadi ya Mashahidi Ugiriki ilikuwa imeongezeka hadi zaidi ya 4,000, na majengo yaliyopanuliwa yalihitajika. Hivyo, tulihamia Betheli mpya yenye orofa tatu mjini Athene kwenye Kartali Street.

  • “Badala ya Dhahabu, Nilipata Almasi”
    Mnara wa Mlinzi—1997 | Machi 1
    • Pia tulianza tena utendaji wetu wa ukawaida wa uchapaji kwenye majengo ya tawi. Likiwa tokeo, majengo ya Betheli ya Kartali Street upesi yakawa madogo mno. Kwa hiyo, shamba la hektari moja lilinunuliwa katika kiunga cha Athene cha Marousi. Majengo mapya ya Betheli yalijengwa yaliyokuwa na vyumba 27 vya kulala, kiwanda, ofisi, na majengo mengine. Haya yaliwekwa wakfu katika Oktoba 1979.

      Hatimaye tulihitaji hata nafasi zaidi. Kwa hiyo shamba la hektari 22 lilinunuliwa karibu kilometa 60 kaskazini ya Athene. Hapo mahali pako katika Eleona, kwenye upande wa kilima palipo na mandhari ya milima na mabonde yenye maji mengi. Hapo, katika Aprili 1991, tuliweka wakfu jengo kubwa zaidi lililo na nyumba 22, ambazo kila mojawapo yaweza kutosha kwa watu wanane.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki