-
Matukio Muhimu ya Mwaka Uliopita2010 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
Jumamosi Mei 2, 2009, ndugu na dada wapatao 600 kutoka nchi 31 walisikiliza hotuba ya kuweka wakfu kwenye ofisi ya tawi ya Uholanzi iliyotolewa na Theodore Jaracz wa Baraza Linaloongoza. Sehemu ya makao iliongezwa kwenye jengo lililojengwa 1983, nayo majengo yaliyotumiwa kuchapa magazeti yakafanyiwa marekebisho na kuwa ofisi na Kituo cha Kutayarisha na Kurekodi CD na DVD. Kituo hicho kinatumiwa kutayarisha CD na DVD katika lugha 24, na nyingi kati ya hizo zinazungumzwa barani Ulaya. Isitoshe, ndugu kwenye kituo hicho wanasaidia kutayarisha video katika lugha 20 za ishara. Kazi hiyo inahusisha kusimamia utayarishaji wa CD barani Ulaya, Afrika, na Visiwa vya Bahari ya Pasifiki, na utayarishaji wa DVD ulimwenguni kote. Ofisi ya tawi ya Uholanzi pia hununua na kusafirisha vifaa vinavyohitajiwa na ofisi katika sehemu nyingine za ulimwengu, na majengo hayo yaliyofanyiwa marekebisho yanafaa sana kwa kazi hiyo.
-
-
Matukio Muhimu ya Mwaka Uliopita2010 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
[Picha katika ukurasa wa 28]
Ndugu Jaracz akitoa hotuba ya kuweka wakfu kwenye ofisi ya tawi ya Uholanzi
-