-
Mashahidi wa Yehova Nchini UrusiAmkeni!—1997 | Agosti 22
-
-
Sergei Ivanenko, mwanatheolojia Mrusi aheshimiwaye, alifanya vivyo hivyo. Ingawa aliamini nyingi za ripoti hasi kuhusu Mashahidi wa Yehova ambazo zilikuwa zikisambaa nchini Urusi, aliamua kuulizia ofisi ya tawi ya Mashahidi, ambayo ilikuwa nje tu ya St. Petersburg, ili apate habari. Alikubali mwaliko wa kuzuru huko, aulize maswali, na ajionee mwenyewe Mashahidi.
Bw. Ivanenko alipofika mnamo Oktoba 1996, majengo ambayo ni makao ya washiriki karibu 200 wa wafanyakazi wa ofisi ya tawi ya Mashahidi wa Yehova nchini Urusi yalikuwa yakikaribia ukamilisho. Kwa siku tatu zilizofuata, alipewa fursa ya kupatazama mahali hapo pa ujenzi, kula milo katika chumba cha mlo, na kuhoji mtu awaye yote ambaye angependa.
-
-
Mashahidi wa Yehova Nchini UrusiAmkeni!—1997 | Agosti 22
-
-
“Ili nipate jibu, nilizuru kijiji cha Solnechnoye, katika wilaya ya Kururtnoye, St. Petersburg, ambapo kipo kitovu cha usimamizi cha Mashahidi wa Yehova nchini Urusi.
***
“[Hapa] ni mahali ambapo zamani palikuwa kambi ya wakati wa kiangazi. Kufikia 1992 jengo [la awali] lilikuwa limechakaa sana, na badala ya watoto waliokuwa wakicheza kukawa na makundi ya panya. Yaonekana kwamba ni hali mbaya sana ya eneo hili iliyofanya Mashahidi wa Yehova wapokee ploti ya hekta saba [eka 17] watumie kwa muda usio dhahiri. Walirekebisha upya majengo ya zamani na kuanza kujenga majengo mapya, kutia ndani jengo la usimamizi lenye orofa nne, [Jumba la Ufalme] linalotoshea watu 500, na chumba cha kulia. Mashahidi wa Yehova pia wanapanda nyasi mpya (ambazo ziliagizwa rasmi kutoka Finland) na aina kadhaa za miti iliyo nadra kupatikana. Hiyo kazi inatazamiwa kukamilishwa katika kiangazi hiki kinachokuja. Kazi kubwa ya kitovu cha usimamizi ni kupanga utendaji wa kuhubiri na kusafirisha fasihi kwenye makutaniko ya mahali-mahali ya Mashahidi wa Yehova. Solnechnoye haina vifaa vyake vya uchapishaji, kwa hiyo fasihi za Kirusi huchapishwa Ujerumani, kisha hupelekwa St. Petersburg, na kutoka huko hizo husambazwa kwa maeneo mbalimbali. Watu wapatao 190 hufanya kazi katika kitovu hicho. Wao hufanya kazi kwa kujitolea na ingawa hawapokei mishahara, wao huandaliwa mahitaji yote ya kimsingi, kama vile mahali pa kuishi, chakula, na mavazi.
“Kazi ya kitovu hicho inaongozwa na halmashauri ya wazee 18. Vasily Kalin amekuwa mratibu wa hicho kitovu cha usimamizi tangu 1992. Alizaliwa katika Ivano-Frankovsk. Mnamo 1951, akiwa na umri wa miaka minne, yeye pamoja na wazazi wake walihamishwa Siberia (mwaka wa 1949 na 1951 familia zipatazo 5,000 zilinyanyaswa na wenye mamlaka kwa sababu ya kuwa Mashahidi wa Yehova). Alibatizwa mwaka wa 1965 na kuishi eneo la Irkutsk. Alikuwa mnyapara katika kiwanda cha mbao.
“Mbali na wajitoleaji wa hicho kitovu cha usimamizi kuna wafanyakazi wa ujenzi wenye kujitolea 200 ambao wametoka Urusi, Finland, Sweden na Norway wanaoishi Solnechnoye: Wengi wao walichukua likizo kutoka kwa kazi zao za kawaida. Pia kuna Mashahidi wa Yehova wengi kutoka Ukrainia, Moldova, Ujerumani, Marekani, Finland, Poland na nchi nyinginezo. (Mashahidi wa Yehova hawana ubaguzi wa kijamii. Japo uhakika wa kwamba Wageorgia, Waabkhazian, Waazerbaijan na Waarmenia wanaishi pamoja katika kitovu hicho, hakujapata kuwa na mgogoro wowote kwa miaka minne.)
“Vingi vya vifaa vya ujenzi vilitolewa na nchi za Skandinavia, na vingine vingi vilitolewa bila malipo na waamini wenzao. Nilionyeshwa buldoza ambayo Shahidi wa Yehova wa Sweden aliileta Solnechnoye mwaka wa 1993. Yeye aliitumia muda wote alipokuwa huko, na kabla ya kwenda nyumbani aliwapa ndugu zake katika imani. Wajenzi wanaishi katika mabweni mazuri na nyumba nzuri ndogondogo. Siku yao hufuata ratiba kama hii: saa 1:00 asubuhi—kiamsha kinywa na sala; wao hufanya kazi tokea saa 2:00 asubuhi hadi saa 11:00 jioni kukiwa na kipindi cha saa nzima cha mlo wa mchana. Siku za Jumamosi wao hufanya kazi mpaka wakati wa mlo wa mchana, na Jumapili ni siku ya kupumzika.
“Wao hula vizuri na sikuzote matunda ni sehemu ya mlo. Dini hii haifungi wala kukataza kabisa kula vyakula fulani kamwe. Baada ya kazi, wengi huenda kuoga kwenye bafu za mvuke na kisha kunywa bia moja au kuketi tu kusikiliza muziki. Hakuna walevi miongoni mwa Mashahidi wa Yehova, lakini alkoholi haikatazwi. Waamini hukubaliwa kunywa kwa kiasi divai, brandi, vodka na kadhalika. Lakini, Mashahidi wa Yehova hawavuti sigareti.
-
-
Mashahidi wa Yehova Nchini UrusiAmkeni!—1997 | Agosti 22
-
-
[Picha katika ukurasa wa 23]
Sehemu ya jengo la ofisi ya tawi nchini Urusi
[Picha katika ukurasa wa 24]
Jumba la Ufalme ambako familia ya ofisi ya tawi nchini Urusi hukutanikia kwa ajili ya funzo la Biblia
-