-
Kutokeza Fasihi za Biblia Ili Zitumiwe Katika HudumaMashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
Vituo vya Duniani Pote ili Kutangaza Kweli ya Biblia
Katika miaka ya mwisho ya 1960 na baada ya hapo, jitihada nyingi zilifanywa ili kutawanya zaidi shughuli za uchapaji za Watch Tower Society badala ya kuwa mahali pamoja. Ukuzi wa idadi ya Mashahidi wa Yehova ulikuwa wa haraka sana. Nafasi zaidi ya kiwanda ilihitajiwa ili kuandaa fasihi za Biblia kwa utumizi wao na kwa kugawanyia umma. Lakini upanuzi katika Brooklyn ulikuwa wa mwendo wa polepole kwa sababu ya nafasi ndogo iliyopatikana pamoja na kulazimika kufuata utaratibu mwingi wa kiofisi serikalini. Mipango ilifanywa ili kufanya uchapaji mwingi kwingineko.
-
-
Kutokeza Fasihi za Biblia Ili Zitumiwe Katika HudumaMashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
Katika mwaka uo huo, 1992, si kwamba tu Watch Tower Society ilikuwa ikichapa fasihi za Biblia katika lugha 180 katika Marekani bali pia viwanda vyayo vikubwa vinne vya kuchapia katika Amerika ya Latin vilikuwa vikiandaa fasihi nyingi zilizohitajiwa nchini humo na pia katika nchi nyinginezo katika sehemu hiyo ya ulimwengu. Viwanda vingine 11 vilikuwa vikitokeza fasihi katika Ulaya, na zote hizo zilikuwa zinasaidia kujazia uhitaji wa fasihi wa nchi nyinginezo. Kati ya hizo, Ufaransa ilikuwa ikitoa fasihi kwa nchi 14, na Ujerumani, ambayo ilichapa katika lugha zaidi ya 40, ilikuwa ikisafirisha ugavi mkubwa kwa nchi 20 na ugavi mdogo zaidi kwenye nchi nyinginezo nyingi. Barani Afrika, viwanda sita vya kuchapia vya Watch Tower vilikuwa vikitokeza fasihi za Biblia katika jumla ya lugha 46. Viwanda vingine 11 vya kuchapia—vingine vikubwa, vingine vidogo—vilikuwa vikiandalia Mashariki ya Kati na Mashariki ya Mbali, visiwa vya Pasifiki, Kanada, na maeneo mengineyo fasihi za kutumia katika kueneza ujumbe wenye uharaka kuhusu Ufalme wa Mungu. Katika nchi 27 nyingine, Sosaiti ilikuwa ikichapa vitu vidogovidogo vilivyohitajiwa na makutaniko ili yatende kazi vema.
-
-
Kutokeza Fasihi za Biblia Ili Zitumiwe Katika HudumaMashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
Ingenufaisha kufanya kazi hiyo katika nchi zilizo nje ya Marekani na kufanywa na ndugu zetu wenyewe huko badala ya mashirika ya kibiashara. Hivyo, iwapo tatizo la ulimwenguni la wakati ujao au kuingiliwa kwa kazi ya Mashahidi wa Yehova na serikali kungezuia shughuli katika sehemu yoyote ya dunia, chakula cha kiroho cha maana bado kingeandaliwa.
Hivyo katika 1971, karibu miaka miwili kabla ya kiwanda cha kwanza cha Watch Tower katika Wallkill kuanza kufanya kazi, kazi ilianzishwa ili kuandaa kiwanda kipya kifaacho cha kuchapa katika Numazu, Japani. Ongezeko la zaidi ya mara tano la wapiga-mbiu wa Ufalme katika Japani wakati wa mwongo uliotangulia lilionyesha kwamba fasihi nyingi za Biblia zingehitajiwa huko. Wakati uo huo, majengo ya tawi katika Brazili yalikuwa yakipanuliwa. Ilikuwa hivyo pia katika Afrika Kusini, ambako fasihi za Biblia zilikuwa zikitokezwa katika lugha nyingi za Kiafrika. Mwaka uliofuata, 1972, vifaa vya kuchapa vya Sosaiti katika Australia viliongezwa mara nne zaidi kwa ukubwa, wakiwa na kusudi la kuandaa kila toleo la Mnara wa Mlinzi na Amkeni! katika sehemu hiyo ya ulimwengu bila kuchelewesha usafirishaji. Viwanda vya ziada vilijengwa pia katika Ufaransa na Filipino.
Mapema katika 1972, N. H. Knorr na mwangalizi wa kiwanda cha Brooklyn, M. H. Larson, walifanya ziara ya kimataifa ili kuchunguza kazi iliyokuwa ikifanywa, ili kupanga mambo kwa utumizi bora zaidi wa vifaa hivyo na kuweka msingi kwa ajili ya upanuzi zaidi ambao ungefuata. Ziara zao zilitia ndani nchi 16 katika Amerika Kusini, Afrika, na Mashariki ya Mbali.
Punde baadaye, ofisi ya tawi katika Japani ilikuwa ikitokeza yenyewe magazeti katika lugha ya Kijapani yaliyohitajika katika sehemu hiyo ya shamba, badala ya kutegemea wachapaji wa kibiashara. Mwaka uo huo, 1972, ofisi ya tawi katika Ghana ilianza kuchapa Mnara wa Mlinzi katika lugha tatu kati ya lugha za wenyeji, badala ya kungoja safirisho kutoka Marekani na Nigeria. Halafu, ofisi ya tawi ya Filipino ilianza kushughulikia utungaji na uchapaji wa Mnara wa Mlinzi na Amkeni! katika lugha nane za wenyeji (kutia na kuchapa magazeti yaliyohitajika katika lugha ya Kiingereza). Hiyo ilikuwa hatua kubwa sana katika kutawanya shughuli za uchapaji za Watch Tower.
Kufikia mwisho wa 1975, Watch Tower Society ilikuwa ikichapa fasihi za Biblia katika vifaa vyayo yenyewe katika nchi 23 duniani pote—vitabu katika nchi tatu; vijitabu au magazeti au yote mawili katika sehemu zote 23. Sosaiti ilikuwa ikitokeza tena vitu vidogovidogo zaidi katika vifaa vyayo yenyewe, katika nchi 25.
-