Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Afrika Kusini
    2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • MRADI MKUBWA

      Nathan Knorr na Milton Henschel, ambao walikuwa wakitumikia katika makao makuu huko Brooklyn, walipotembelea Afrika Kusini mwaka wa 1948, iliamuliwa kwamba uwanja ununuliwe wa kujenga makao ya Betheli na kiwanda cha uchapaji huko Elandsfontein karibu na Johannesburg. Mradi huo ulimalizika mwaka wa 1952. Kwa mara ya kwanza, Wanabetheli wote wangeweza kukaa katika jengo moja. Mashini nyingi zaidi za kuchapisha zilianza kutumiwa, kutia ndani mashini bapa ya kuchapa. Gazeti la Mnara wa Mlinzi lilichapishwa katika lugha nane na Amkeni! katika lugha tatu.

  • Afrika Kusini
    2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Mwaka wa 1959, makao ya Betheli na majengo ya kiwanda yakapanuliwa. Majengo yaliyoongezwa yalikuwa makubwa kuliko ya awali. Mashini mpya ya kuchapa inayoitwa Timson ilianza kutumiwa. Hiyo ndiyo mashini ya kwanza yenye mtambo wa kuzunguka ambayo ilitumiwa katika ofisi hiyo ya tawi.

      Ili kuwasaidia kutumia mashini hizo, Ndugu Knorr aliwaalika vijana wanne kutoka Kanada wahamie Afrika Kusini: Bill McLellan, Dennis Leech, Ken Nordin, na John Kikot. Waliwasili Novemba 1959. Bill McLellan na mke wake, Marilyn, wangali wanatumika katika Betheli ya Afrika Kusini, John Kikot na mke wake, Laura, sasa wanatumikia katika Betheli ya Brooklyn, New York. Ken Nordin na Dennis Leech waliendelea kukaa Afrika Kusini, wakaoa na kupata watoto. Wanaendelea kuchangia pakubwa katika kazi ya Ufalme. Watoto wote wawili wa Ken wanatumikia katika Betheli ya Afrika Kusini.

      Betheli iliyopanuliwa na majengo mapya yalitumiwa vizuri kushughulikia ongezeko nchini. Mwaka wa 1952, idadi ya wahubiri nchini Afrika Kusini ilizidi 10,000. Kufikia 1959, idadi hiyo ilikuwa imeongezeka hadi 16,776.

  • Afrika Kusini
    2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Ofisi ya tawi ya kwanza ilipojengwa huko Elandsfontein, wenye mamlaka hawakuruhusu akina ndugu weusi, machotara, na Wahindi waishi katika jengo moja na ndugu wazungu. Wakati huo, Wanabetheli wengi walikuwa wazungu kwa sababu ilikuwa vigumu kwa watu wa jamii nyingine kupata vibali vya kufanya kazi jijini. Hata hivyo, kulikuwa na ndugu na dada 12 weusi na machotara Betheli, hasa watafsiri wa lugha za kienyeji. Serikali ilitoa kibali ndugu hao wajengewe vyumba vitano nyuma na kando ya majengo makuu ya kukaa. Baadaye, kibali hicho kilifutwa wakati sheria za ubaguzi wa rangi zilipoanza kutekelezwa hata zaidi, na ndugu zetu walilazimika kusafiri hadi maeneo ya watu weusi yaliyokuwa karibu, umbali wa kilomita 20 hivi ili kukaa katika mabweni ya wanaume. Dada wawili weusi waliishi katika nyumba za Mashahidi wengine katika maeneo hayo.

      Sheria hata haikuwaruhusu Wanabetheli hao wale chakula pamoja na ndugu zao wazungu katika chumba cha kulia chakula, na wapelelezi wa baraza la jiji walichunguza kuona iwapo sheria hiyo ilivunjwa. Hata hivyo, ndugu hao wazungu hawakuvumilia jambo hilo. Hivyo basi, walibadili vioo vya madirisha na kuweka vioo visivyoonyesha wazi katika chumba hicho ili waweze kula pamoja wakiwa familia nzima bila kusumbuliwa.

  • Afrika Kusini
    2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Mwaka wa 1971, Ndugu Knorr alitembelea tena Afrika Kusini. Kufikia wakati huo, Betheli ilikuwa imejaa tena. Kulikuwa na Wanabetheli 68. Basi, mipango ya kupanua majengo ilifanywa, na ndugu walijitolea kufanya kazi au kutoa michango kwa ajili ya kazi hiyo. Ujenzi ulimalizika Januari 30, 1972. Baadaye, upanuzi mwingine ulifanywa, nao ukakamilishwa mwaka wa 1978. Upanuzi wote huo ulitia moyo na kuonyesha wazi utegemezo wa Yehova, kwa sababu wakati huo watu wa Mungu walipingwa sana na wenye mamlaka.

  • Afrika Kusini
    2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • [Picha katika ukurasa wa 108, 109]

      ya awali, 1952

      Betheli, Elandsfontein, 1972

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki