Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Albania
    2010 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Wakati huo kulikuwa na wahubiri 2,200 nchini Albania nayo familia ya Betheli ilikuwa na watu 40. Nyumba za kukaa zilikuwa zimekodishwa, hata hivyo, vyumba zaidi vilihitajika. Hivyo, Baraza Linaloongoza liliidhinisha uwanja wa ekari saba ununuliwe viungani vya mji wa Tiranë katika eneo la Mëzez. Ili kusimamia vizuri zaidi eneo kubwa zaidi la Albania na Kosovo, Halmashauri ya Nchi ikawa Halmashauri ya Tawi mwaka wa 2000.

      Septemba 2003, ujenzi wa ofisi mpya ya tawi ulipoanza, Albania ilikuwa na wahubiri 3,122.

  • Albania
    2010 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • KUWEKWA WAKFU KWA OFISI YA TAWI

      Mnamo Juni 2006, Theodore Jaracz na Gerrit Lösch wa Baraza Linaloongoza, walikuwa miongoni mwa wajumbe 350 kutoka katika nchi 32 waliohudhuria programu ya kuweka wakfu ofisi mpya ya tawi. Mwingine aliyehudhuria programu hiyo ni Sotir Ceqi, aliyekuwa ameteswa kwa kupigwa kwa umeme katika miaka ya 1940. Sasa, akiwa na umri unaokaribia miaka 80, angali akitumikia kwa shangwe.

      “Siku hii ni kama ndoto,” akasema Frosina Xheka, ambaye angali akitumikia kwa uaminifu licha ya magumu ya miaka mingi. Polikseni Komino, mjane wa Jani, alihudhuria, naye alisimulia kuhusu binti na wajukuu zake, ambao ni mapainia wa kawaida. Vasil Gjoka pia alikuwako, akitembea kana kwamba ana kibyongo kwa sababu ya kuteseka kwa miaka mingi. Machozi yalimlengalenga alipokumbuka safari ya kwenda kumtembelea Leonidha Pope na kubatizwa kisiri mwaka wa 1960.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki