-
Estonia2011 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
Mwaka huohuo, Waziri wa Mambo ya Ndani alifunga Shirika la Watch Tower nchini Estonia, akatwaa vitabu, na kuweka mali ya shirika hilo chini ya umiliki wa serikali.
-
-
Estonia2011 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
Wakati huohuo, kazi ya kuhubiri iliendelea, na kazi katika ofisi ikaanza tena. Vitabu kadhaa viliendelea kutwaliwa katika miaka iliyofuata. Hellin Aaltonen alikuwa akifanya kazi katika ofisi ya tawi wakati uvamizi fulani ulipofanywa.
“Polisi watatu vijana walikuja hasa kutwaa kijitabu Millions Now Living Will Never Die!” asema Dada Aaltonen, “lakini hatukuwa na nakala zozote. Walitoa vitabu vyote kwenye rafu na kuvitupa sakafuni. Ndugu Baxter hangeweza kufanya lolote, kwa kuwa walikuwa wanamwangalia kwa makini. Nilianza kupanga vile vitabu na bila kuonekana nikaenda kwenye dawati la Ndugu Baxter kuangalia kama kuna karatasi zozote ambazo polisi hao hawakupaswa kuziona. Niliona barua iliyokuwa na majina na anwani za wahubiri wote, nami nikaitupa kwenye kapu la takataka lililokuwa pembeni. Polisi hao walipoanza kupakia vitabu katika masanduku, msimamizi wao alichukua sanduku moja kwa kiburi na kulirusha kwa nguvu sana hivi kwamba mkono wake ulivunjika! Hivyo, polisi hao wakaondoka upesi kumpeleka hospitalini, nasi tukapata nafasi ya kupekua masanduku yote kabla hawajarudi.”
Ndugu Baxter anaongeza, “Polisi hao walirudi na walipokuwa wakipakia vitabu hivyo, nikamwona mmoja wao akiweka kitabu Deliverance kwenye mfuko wa koti lake. Mara kwa mara mimi nimejiuliza ni vitabu vingine vingapi ambavyo maofisa hao walichukua na kusoma?”
-