Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Nilisaidiwa Kuacha Kuwa Mwenye Haya
    Mnara wa Mlinzi—2000 | Juni 1
    • Tulipofika na Martha Japani kwa mara ya kwanza, tulipewa mgawo wa kuishi kwenye ofisi ya tawi jijini Tokyo. Mwaka wa 1963, ofisi mpya yenye orofa sita ilijengwa mahali hapo, na tumeishi hapo tangu wakati huo hadi sasa. Mnamo Novemba 1963 tulikuwa miongoni mwa wale 163 waliosikiliza hotuba ya kuweka wakfu iliyotolewa na msimamizi wa tawi, Lloyd Barry. Kufikia wakati huo tulikuwa Mashahidi 3,000 nchini Japani.

      Imependeza sana kuona kazi ya kuhubiri juu ya Ufalme ikikua haraka sana, tukifikia zaidi ya Mashahidi 14,000 mwaka wa 1972 wakati ambapo ofisi mpya ya tawi iliyoongezwa ilimalizika katika jiji la Numazu. Lakini, kufikia mwaka wa 1982 kulikuwa na watangazaji wa Ufalme zaidi ya 68,000 nchini Japani, na ofisi kubwa zaidi ilijengwa katika jiji la Ebina, kilometa 80 hivi kutoka Tokyo.

  • Nilisaidiwa Kuacha Kuwa Mwenye Haya
    Mnara wa Mlinzi—2000 | Juni 1
    • Jambo kuu katika maisha yangu ya mishonari lilitukia mwezi wa Novemba uliopita, miaka 36 baada ya kuwekwa wakfu kwa jengo ambamo wengi wetu sisi mishonari twaishi sasa. Novemba 13, 1999, nilikuwa miongoni mwa watu 4,486, kutia ndani mamia ya Mashahidi wa zamani kutoka nchi 37, waliohudhuria kuwekwa wakfu kwa majengo yaliyoongezwa ya ofisi ya tawi ya Japani ya Watch Tower Bible and Tract Society katika Ebina. Kwa wakati huu, kuna watu wapatao 650 katika ofisi hiyo ya tawi.

  • Nilisaidiwa Kuacha Kuwa Mwenye Haya
    Mnara wa Mlinzi—2000 | Juni 1
    • [Picha katika ukurasa wa 25]

      Majengo ya ofisi ya tawi yaliyoongezwa katika Ebina yaliwekwa wakfu mwezi wa Novemba uliopita

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki