Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kujenga Pamoja Duniani Pote
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • Tawi la Japani lilikuwa limehamia Numazu kutoka Tokyo kwenye makao makubwa mapya katika 1972. Upanuzi zaidi uliokuwa mkubwa ulifanywa katika 1975. Kufikia 1978 mahali pengine palikuwa pamenunuliwa, katika Ebina; na kazi ya kujenga kiwanda kilichozidi ukubwa wa kile kilicho Numazu kwa mara tatu ilianza haraka. Hicho kilikamilishwa katika 1982. Bado hakikutosha; majengo zaidi yaliongezwa kufikia 1989. Je, haingewezekana kujenga mara moja tu na kukifanya kiwe kikubwa vya kutosha? La. Idadi ya wapiga-mbiu wa Ufalme katika Japani imerudufika tena na tena kwa njia ambayo hakuna mtu angeweza kutazamia. Kuanzia 14,199 katika 1972, idadi yao imepanda hadi 137,941 katika 1989, na walio wengi wao walikuwa katika huduma ya wakati wote.

  • Kujenga Pamoja Duniani Pote
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • Maadamu watu si wakamilifu, kutakuwako matatizo, lakini wale ambao hufanya kazi kwenye ujenzi huo hujaribu kutatua matatizo kwa msingi wa kanuni za Biblia. Wanajua kwamba kufanya mambo katika njia ya Kikristo ni jambo la maana zaidi ya kuwa na matokeo. Kikiwa kikumbusho, kwenye mahali pa ujenzi katika Ebina, Japani, kulikuwa ishara kubwa zenye picha za wafanyakazi wenye kuvalia kofia ngumu, na juu ya kila kofia ngumu liliandikwa kwa herufi za Kijapani moja la matunda ya roho ya Mungu: upendo, shangwe, amani, ustahimilivu, fadhili, wema, imani, upole, kujidhibiti. (Gal. 5:22, 23, NW)

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki