-
Matunda ya Pekee Kutoka AmazoniAmkeni!—2004 | Julai 22
-
-
Mti wa Bacuri na Cupuaçu
Mti wa bacuri (Platonia insignis) ni maridadi, na una urefu wa kati ya meta 20 na 30. Matawi yake ya juu yana umbo la pia iliyopinduliwa. Ukubwa wa tunda hilo umekaribiana na ule wa chungwa na lina umbo la yai na ngozi nzito ya manjano. Tabaka lake jeupe linalofunika mbegu huwa tamu na chungu, lenye kunata, na lenye harufu nzuri. Tabaka hilo lenye umajimaji huwa na fosforasi, chuma, na vitamini C nyingi. Wabrazili husaga bacuri kutengeneza shira, jeli, rojo, na vinywaji. Mbegu zake nyeusi zenye wekundu-wekundu na zenye mafuta hazitupwi bali hutumiwa kutibu magonjwa ya ngozi. Mbao za manjano za bacuri hutumiwa katika ujenzi.
-
-
Matunda ya Pekee Kutoka AmazoniAmkeni!—2004 | Julai 22
-
-
[Picha katika ukurasa wa 16]
Matunda ya “Bacuri,” na mti upande wa kushoto
[Hisani]
Bacuri fruit: Geyson Magno/Ag. Lumiar
-