Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Ndoa ya Kidesturi” Katika Ghana
    Amkeni!—1996 | Desemba 8
    • Katika Ghana namna ya kawaida sana ya ndoa ni ile iitwayo ndoa ya kidesturi. Hii huhusisha familia ya bwana-arusi kulipa mahari kwa familia ya bibi-arusi. Ndoa ya kidesturi huzoewa na watu katika sehemu kubwa ya Afrika na katika mahali kama vile Hong Kong, Papua New Guinea, na Visiwa vya Solomon na vilevile miongoni mwa Wahindi wa Goajiro katika kaskazini-mashariki mwa Kolombia na kaskazini-magharibi mwa Venezuela, kutaja mahali pachache tu.

      Kulipwa kwa mahari kulikuwa desturi katika nyakati za Biblia. (Mwanzo 34:11, 12; 1 Samweli 18:25) Ufahamu katika nyakati za kale na leo ni kwamba mahari ni fidia kwa wazazi wa msichana kwa sababu ya wao kupoteza utumishi wake na kwa wakati, nishati, na mali zilizotumiwa katika elimu na kutunzwa kwake kabla ya ndoa.

  • “Ndoa ya Kidesturi” Katika Ghana
    Amkeni!—1996 | Desemba 8
    • Idadi ya watu ambao hukusanyika kwenye nyumba ya msichana au nyumba ya mwakilishi aliyechaguliwa kwa ajili ya kulipwa kwa mahari, tukio ambalo hufanyiza ndoa, kwa kawaida huwa kubwa kuliko idadi ya walioko katika sherehe ya kubisha mlango. Hii ni kwa sababu marafiki wengi sasa wapo.

      Mazingira ni yenye shangwe. Wanaume na wanawake vijana walio waseja wana hamu ya kuona kile ambacho kimeletwa kwa bibi-arusi. Lakini mazingira hayo yenye furaha hupata mkazo wakati familia ya bibi-arusi ilalamikapo kwamba bidhaa za mahari hazijakamilika. Baadhi ya watazamaji huwa na wasiwasi wa litakalotokea wakati familia ya bibi-arusi ionekanapo kuwa ngumu. Msemaji wa bwana-arusi hubishana kwa ustadi ili aonewe huruma na familia ya bibi-arusi. Hali hutulia wakati familia ya msichana inapokubali. Kisha mazingira yabadilika tena. Sasa mazingira ni ya kusherehekea, na vitafuno tofauti-tofauti vyaandaliwa.

      Ili kuanza sherehe ya ndoa, msemaji wa bibi-arusi awatuliza waliokusanyika na kuwakaribisha wote. Awauliza wawakilishi wa bwana-arusi kuhusu utume wao. Msemaji wa bwana-arusi ataja sababu yao ya kuja, akikumbusha waliokusanyika kwamba tayari mlango ulibishwa na kwamba kuna ruhusa ya kuingia.

      Kisha kila msemaji wa familia awajulisha waliokusanyika washiriki wa karibu wa familia, kutia ndani yule anayepeana mkono wa msichana na vilevile yule anayetegemeza mvulana kuhusiana na ndoa hiyo. Sherehe yaendelea.

      MM: [Akiwazungumzia wawakilishi wa bwana-arusi] Tafadhalini toeni bidhaa za ndoa tulizowaomba.

      Msemaji wa bibi-arusi ataja bidhaa moja-moja za mahari ili wote wahakikishe kwamba zipo. Wawakilishi wa bwana-arusi wakihisi kwamba familia ya bibi-arusi imepandisha madai, wao wanatatua suala hilo faraghani kabla ya siku ya ndoa. Hata hivyo, familia ya bwana-arusi huja kwenye sherehe hiyo wakiwa tayari kupigania kupunguzwa kwa ziada zozote ikiwa familia ya bibi-arusi yathibitika kuwa ngumu. Mahali popote anapoishi mtu, mahari ya msingi—iwe ya juu au ya chini—ni lazima ilipwe yote.

      Familia fulani hudai zipewe vitu kama vile, vinywaji, nguo, mikufu, vipuli, na vitu vingine vya mabibi. Katika kaskazini mwa Ghana, mahari yaweza kutia ndani chumvi, njugu aina ya kola, kanga (ndege), kondoo, na hata ng’ombe. Kuna sehemu ya mahari ya fedha taslimu isiyoepukika.

      Makubaliano yanapokuwa yakiendelea, bibi-arusi hayupo lakini yuko karibu, akitazama. Bwana-arusi aweza kuchagua kuwapo au kutowapo. Hivyo, mtu anayeishi mbali sana aweza kuwapa wazazi wake idhini ya kufanya mkataba wa ndoa kwa niaba yake. Hata hivyo, kwa pindi inayofafanuliwa hapa, bwana-arusi yupo. Sasa ni zamu ya familia yake kufanya madai.

      MMV: Tumetimiza yote tuliyotakikana kutimiza, lakini hatujamwona binti-mkwe wetu.

      Sherehe ya ndoa si shughuli yenye uzito sana; pia ni pindi ya kufurahi. Familia ya msichana sasa yaitikia madai ya familia ya mvulana ya kumwona bibi-arusi.

      MM: Twatamani kwamba bibi-arusi angekuwa hapa. Kwa kuhuzunisha, amesafiri kwenda ng’ambo na hatuna pasipoti au viza za kusafiri kwenda kumleta.

      Kila mtu ajua kinachomaanishwa na hilo. Mara moja, familia ya bwana-arusi yatoa kiasi fulani cha fedha—kiasi chochote awezacho kutoa bwana-arusi—na ghafula! pasipoti na viza za kuwaziwa ziko tayari. Na bibi-arusi amerudi kutoka safari yake ya kuwaziwa!

      Ili kuongezea raha, makabila fulani hupanga kwamba marafiki fulani wajifanye kuwa bibi-arusi. Kila anayejifanya kuwa bibi-arusi anakataliwa na umati hadi, huku wakipiga makofi mazito, bibi-arusi wa kweli anatolewa. Kisha anaalikwa na msemaji wake atazame bidhaa kadhaa za mahari yake. Anaulizwa ikiwa kile ambacho bwana-arusi ameleta chapaswa kukubaliwa. Kuna kimya huku kila mtu akingoja jibu kwa wasiwasi. Wasichana fulani ni waoga na wengine wajasiri, lakini sikuzote jibu huwa ndiyo, likifuatwa na makofi mazito.

      Bwana-arusi akiwapo, familia ya bibi-arusi hutaka imjue. Raha inaendelea bila kukomeshwa kukipangwa mmoja wa rafiki zake ajifanye kuwa bwana-arusi. Akijichukua kwa kujisikia, rafiki yake asimama, lakini mara moja kila mtu apaaza sauti za kumkataa.

      Wazazi wa bibi-arusi tena wadai kumwona mwana-mkwe wao. Bwana-arusi wa kweli sasa asimama, akitabasamu kwa furaha. Familia ya bibi-arusi yamruhusu msichana ajiunge na mume wake, ambaye hutia pete kwenye kidole chake ikiwa pete ilikuwa sehemu ya mahari. Pete ni wazo la kutoka Magharibi. Naye pia, atia pete kwenye kidole cha bwana-arusi. Pongezi na shangwe zajaa. Kwa ajili ya kufaa kwa hali na kupunguza gharama, watu fulani sasa huunganisha sherehe ya kubisha mlango pamoja na kufunga ndoa katika siku moja.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki