Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kujinyima Chakula na Kuwa na Hamu ya Chakula Isiyo ya Kawaida—Mambo Hakika, Hatari
    Amkeni!—1999 | Januari 22
    • Hamu ya Chakula Isiyo ya Kawaida —Kula kwa Wingi na Kusafisha Tumbo

      Tatizo la kuwa na hamu ya chakula isiyo ya kawaida hutambuliwa na kula kwa wingi (kula upesi kiasi kikubwa cha chakula, labda kalori 5,000 au zaidi) na kisha kusafisha tumbo (kuacha tumbo likiwa tupu, mara nyingi kwa kutapika au kwa kutumia dawa za kuharisha).b

      Kwa kutofautishwa na kujinyima chakula, kuwa na hamu ya chakula isiyo ya kawaida hakutambuliwi kwa urahisi. Huenda mwenye tatizo hili asiwe mwembamba isivyo kawaida, na mazoea yake ya kula yaweza kuonekana kuwa ya kawaida—angalau kwa watu wengine. Lakini kwa mtu aliye na hamu ya chakula isiyo ya kawaida, kwa hakika maisha si ya kawaida. Kwa kweli, yeye huhangaikia chakula kupita kiasi hivi kwamba kila kitu kingine huwa hakina maana. “Kadiri nilivyokula kwa wingi na kutapika, ndivyo nilivyokosa kujali juu ya mambo mengine au watu wengine,” asema Melinda mwenye umri wa miaka 16. “Kwa kweli nilisahau kufurahia ushirika wa marafiki zangu.”

      Geneen Roth, mwandishi na mwalimu katika uwanja wa kitaaluma wa matatizo ya kula, afafanua kula kwa wingi kuwa “kichaa cha dakika thelathini, kuingia kwenye eneo lisilokuwa na vizuizi.” Asema kwamba wakati wa kula kwa wingi, “hakuna kitu kinachokuwa cha maana—si marafiki, si familia . . . Hakuna kitu kinachokuwa cha maana ila chakula.” Lydia mwenye umri wa miaka 17 aliye na tatizo hili afafanua hali yake kwa kutumia mfano ulio wazi. “Ninahisi kuwa kama kifaa cha kuponda takataka,” asema. “Kula chakula kingi, kitafune, kitapike. Kwa kurudia jambo hilo hilo.”

      Mtu mwenye hamu ya chakula isiyo ya kawaida hujaribu sana kuzuia kuongeza uzito ambao kwa kawaida ungeletwa na kula kusikodhibitiwa. Kwa hiyo, mara tu baada ya kula kwa wingi, ama hujaribu kutapika ama kunywa dawa za kuharisha ili kuondoa chakula kabla hakijageuzwa kuwa mafuta ya mwili.c Ingawa wazo hilo laweza kuonekana kuwa lenye kuchukiza, mtu mwenye kula kwa wingi halioni hivyo. “Kadiri unavyokula kwa wingi na kusafisha tumbo, ndivyo iwavyo rahisi kwako,” aeleza mfanyakazi wa huduma za jamii Nancy Kolodny. “Hisi zako za mapema za kuchukizwa au hata hofu hubadilishwa mara moja na kichocheo cha kurudia mambo haya ya kuwa na hamu ya chakula isiyo ya kawaida.”

      Kuwa na hamu ya chakula isiyo ya kawaida ni jambo lililo hatari sana. Kwa kielelezo, kurudia-rudia kusafisha tumbo kwa kutapika hufanya mdomo upatwe na asidi kali za tumbo, ambazo zinaweza kumomonyoa tabaka ya nje ya meno ya mtu mwenye hamu ya chakula isiyo ya kawaida. Zoea hilo pia laweza kuharibu umio, ini, mapafu, na moyo wa mwenye tatizo hili. Katika visa vinavyopita kiasi, kutapika kwaweza kusababisha tumbo lipasuke na hata kifo. Dawa za kuharisha zinapotumiwa kupita kiasi zaweza kuwa hatari pia. Zaweza kuharibu matumbo na pia kusababisha kuharisha mfululizo na kuvuja damu kwa utumbo mpana. Kama vile kutapika mara kwa mara, matumizi mabaya ya dawa za kuharisha, katika visa vinavyopita kiasi, husababisha kifo.

  • Kujinyima Chakula na Kuwa na Hamu ya Chakula Isiyo ya Kawaida—Mambo Hakika, Hatari
    Amkeni!—1999 | Januari 22
    • c Ili wasiongeze uzito, watu wengi wenye hamu ya chakula isiyo ya kawaida hufanya mazoezi kwa bidii kila siku. Baadhi yao hufaulu sana katika kupunguza uzito hivi kwamba baada ya muda hujinyima chakula, na baada ya hapo hali yao yaweza kuwa ikibadilika kati ya kujinyima chakula na kuwa na hamu ya chakula isiyo ya kawaida.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki