-
Yehova—Mungu Aliye Hodari kwa Nguvu ZakeMnara wa Mlinzi—2000 | Machi 1
-
-
c Yaelekea kwamba fahali wa mwitu anayetajwa katika Biblia ni auroch (Kilatini urus). Miaka elfu mbili iliyopita, wanyama hawa waliishi Gaul (ambayo sasa ni Ufaransa), na Juliasi Kaisari aliandika hivi juu yao: “Wanyama hao, uri, karibu watoshane na tembo, lakini tabia yao, rangi yao na umbo lao ni kama fahali. Wana nguvu nyingi sana, na wana mbio sana: hawamwachi mtu wala mnyama mara wanapowaona.”
-
-
Yehova—Mungu Aliye Hodari kwa Nguvu ZakeMnara wa Mlinzi—2000 | Machi 1
-
-
6. Fahali hufananisha nini katika Maandiko, na kwa nini? (Ona kielezi-chini.)
6 Kwa sababu ya nguvu zake, fahali hutumiwa katika Biblia kufananisha uwezo wa Yehova.c Ono la mtume Yohana la kiti cha enzi cha Yehova laonyesha viumbe-hai wanne, na mmojawapo ana uso kama fahali. (Ufunuo 4:6, 7) Inaonekana kwamba mojawapo ya sifa kuu nne za Yehova zinazoonyeshwa na makerubi hao ni nguvu.
-