-
Jiji Kubwa LateketezwaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
20. Ni kielelezo gani kinachoonyesha kujihusisha kwa dini katika mazoea yenye ufisadi ya shughuli za biashara?
20 Kama ilivyotabiriwa na malaika mwenye utukufu, dini imehusika sana katika mazoea yenye ufisadi ya biashara. Mathalani, kuna kujihusisha kwa Vatikani katika anguko la Banco Ambrosiano katika 1982. Kesi hiyo imejikokota muda wote wa miaka ya 1980, lile swali ambalo halijajibiwa likiwa: Fedha zilienda wapi? Katika Februari 1987 mahakimu wa Milani walitoa waranti ili makasisi watatu wa Vatikani wakamatwe, kutia na askofu mkuu mmoja Mwamerika, kwa mashtaka ya kwamba wao walikuwa washiriki kwenye ufilisi wenye udanganyifu, lakini Vatikani ilitupilia mbali ombi la kuwakabidhi wakahukumiwe. Katika Julai 1987, katikati ya makelele ya kuteta, zile waranti zilibatilishwa na Mahakama ya Rufani ya juu zaidi sana kwa msingi wa mwafaka wa zamani kati ya Vatikani na serikali ya Italia.
-
-
Jiji Kubwa LateketezwaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Kwa kutofautisha, dini ya Kibabuloni mara nyingi ina mafungamano mabaya na biashara kubwa-kubwa. Mathalani, katika 1987 Albany Times Union liliripoti kwamba msimamizi wa mambo ya kifedha wa akidayosisi ya Miami, Florida, U.S.A., alikubali kwamba kanisa lina hisa katika makampuni ambayo hufanyiza silaha za nyukilia, sinema zisizofaa, na sigareti.
-
-
Jiji Kubwa LateketezwaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
[Picha katika ukurasa wa 264]
“Wauza-Bidhaa Wasafiri . . . Wakawa na Utajiri”
“Kati ya 1929 na mfyatuko wa Vita ya Ulimwengu 2, [Bernadino] Nogara [msimamizi wa mambo ya kifedha wa Vatikani] aligawia Vatikani jiji kuu na mawakili wa Vatikani kufanya kazi katika maeneo ya namna namna ya uchumi wa Italia—hasa katika nguvu za umeme, mawasiliano ya simu, karidhi na kazi za benki, njia za reli ndogondogo, na ufanyizaji wa zana za kilimo, saruji, na nyuzi za nguo za kubuniwa. Nyingi za shughuli hizi zilifanikiwa.
“Nogara alinyakua kampuni kadhaa kutia na La Società Italiana della Viscosa, La Supertessile, La Società Meridionale Industrie Tessili, na La Cisaraion. Akiunganisha hizi kuwa kampuni moja, ambayo aliita CISA-Viscosa na akaiweka chini ya usimamizi wa Baron Francesco Maria Oddasso, mmojapo makabwela wa Vatikani wenye kuitibariwa zaidi sana, kisha Nogara akaongoza mambo kwa werevu ili kampuni hiyo mpya itwaliwe na [kampuni] ya Italia iliyo kubwa zaidi sana ya kufanyiza nguo, SNIA-Viscosa. Hatimaye faida za Vatikani katika SNIA-Viscosa zikakua zikawa kubwa zaidi na zaidi, na baada ya wakati Vatikani ikachukua udhibiti—kama inavyoshuhudiwa na uhakika wa kwamba baadaye Baron Oddasso akawa makamu wa msimamizi.
“Ndivyo Nogara akapenya ndani ya kiwanda cha nguo. Yeye alipenya ndani ya viwanda vingine katika njia nyingine nyingine, kwa maana Nogara alikuwa mwenye vitimbi vingi. Mtu huyu asiye na ubinafsi . . . pengine alifanya mengi zaidi kutia uhai katika uchumi wa Italia kuliko mwanabiashara mwingine yeyote mmoja katika historia ya Italia . . . Benito Mussolini hakuweza kamwe kupata kabisa milki ambayo yeye aliotea ndoto, lakini yeye aliwezesha Vatikani na Bernadino Nogara kubuni utawala wa aina nyingine.”—The Vatican Empire, cha Nino Lo Bello, kurasa 71-3.
Hiki ni kielelezo kimoja tu cha ushirikiano wa karibu karibu kati ya wauza-bidhaa wa dunia na Babuloni Mkubwa. Si ajabu kwamba wauza-bidhaa hawa wataomboleza wakati mshirika wao wa kibiashara atakapokuwa hayupo tena!
-