Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Tunzeni Akili Zenu Kwa Ukamili”
    Mnara wa Mlinzi—2006 | Machi 1
    • 5. (a) Yeremia alichukua hatua gani ya hekima aliponunua shamba? (b) Kwa nini kuna faida kuandika mapatano yote ya kibiashara katika hati rasmi ya mapatano?

      5 Nabii Yeremia aliponunua shamba kutoka kwa binamu yake, ambaye alikuwa mwabudu mwenzake wa Yehova, aliandika hati ya mapatano mbele ya mashahidi. (Yeremia 32:9-12) Leo, mtu mwenye hekima atahakikisha kwamba mapatano yote ya kibiashara anayofanya, kutia ndani yale anayofanya pamoja na watu wa ukoo na waamini wenzake, yameandikwa katika hati rasmi ya mapatano.a Kuwa na hati ya mapatano iliyoandikwa na kutayarishwa vizuri huzuia hali ya kutoelewana na hudumisha umoja. Kwa upande mwingine, nyakati nyingine watumishi wa Yehova hukosa kuelewana kuhusu mambo ya kibiashara hasa kwa sababu ya kutoandika hati ya mapatano. Kwa kusikitisha, hali hiyo inaweza kusababisha huzuni na chuki, na hata kudhoofisha hali ya kiroho.

  • “Tunzeni Akili Zenu Kwa Ukamili”
    Mnara wa Mlinzi—2006 | Machi 1
    • a Kwa habari zaidi kuhusu kuandika hati ya mapatano ya kibiashara, ona magazeti ya Mnara wa Mlinzi ya Agosti 1, 1997, ukurasa wa 30-31; Novemba 15, 1986, ukurasa wa 16-17; na gazeti la Amkeni! la Agosti 8, 1984, ukurasa wa 13-15, lililochapishwa na Mashahidi wa Yehova.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki