Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Watu Ambao Unaweza Kuwaamini
    Amkeni!—2010 | Oktoba
    • Mfikirie Berthe, mjane anayeishi Kamerun ambaye ana kibanda kidogo cha kuuza vipande vya mihogo vilivyowekwa vikolezo. Anasema: “Kwa kawaida, kuna vipande 20 vya mihogo katika kila pakiti. Wauzaji wengi huweka vipande 17 au 18, lakini mimi sipendi kupata faida kwa kuwadanganya wengine.”

      Je, biashara ya Berthe inamletea faida? Si nyakati zote. Anasema: “Mara nyingi mimi hukaa siku nzima bila kuuza chochote. Lakini ninapowaambia wauzaji chakula kuwa sikuuza chochote na hivyo naomba chakula, wao hunipa kwa kuwa wanajua kwamba nitawalipa mara tu nitakapopata pesa. Wao huniamini kwa sababu nimekuwa mnyoofu sikuzote.”

  • Watu Ambao Unaweza Kuwaamini
    Amkeni!—2010 | Oktoba
    • [Sanduku/Picha katika ukurasa wa 9]

      MIZANI YA UNYOOFU

      Kibanda cha Moïse kinajulikana sana katika soko moja huko Douala, Kamerun ambapo yeye huuza samaki. Anasema: “Nilikiita kibanda changu Mizani kwa sababu mizani ninayotumia ni moja kati ya mizani chache sana sahihi katika soko hilo lote. Ninajua kwamba watu hunijaribu kila wakati. Wakiagiza kilo moja ya samaki, mimi huwapa. Kisha wao huipeleka ikapimwe tena mahali pengine. Inapopimwa, wao huona ni kana kwamba uzani wake unazidi kilo moja! Wanajua kwamba sikuwadanganya! Watu wengi huniambia, ‘Sisi huja kwako kwa sababu wewe ni mnyoofu.’”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki