Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kuhani Mkuu Aliyemhukumu Yesu
    Mnara wa Mlinzi—2006 | Januari 15
    • Kuhani Mkuu Aliyemhukumu Yesu

      KATIKA Novemba 1990, watu waliokuwa wakitengeneza bustani na barabara kilometa moja hivi kusini mwa Jiji la Kale la Yerusalemu walifanya uvumbuzi wenye kustaajabisha. Kwa ghafula, trekta moja iliporomosha dari la pango fulani la kale la kuzikia. Eneo lililokuwa na pango hilo lilitumiwa kuzikia kuanzia karne ya kwanza K.W.K. hadi karne ya kwanza W.K. Uvumbuzi uliofanywa ndani ya pango hilo ulistaajabisha sana.

      Pango hilo lilikuwa na masanduku 12 ya mifupa, na mifupa ya watu waliokufa ilikuwa imeingizwa ndani ya masanduku hayo baada ya kukaa makaburini kwa mwaka mmoja hivi na minofu kuoza. Kando ya sanduku moja lililokuwa limechongwa vizuri ambalo linasemekana kuwa mojawapo ya masanduku bora zaidi kuwahi kupatikana, kulikuwa na jina Yehosef bar Caiapha (Yosefu mwana wa Kayafa).

      Uthibitisho unaonyesha kwamba huenda hilo ndilo kaburi la kuhani mkuu aliyesimamia kesi muhimu zaidi kuwahi kufanywa katika mahakama, yaani, ile ya Yesu Kristo. Mwanahistoria Myahudi Yosefo anamtaja kuhani huyo mkuu kuwa “Yosefu, aliyeitwa Kayafa.” Katika Maandiko, anaitwa tu Kayafa. Kwa nini tupendezwe na habari zake?

  • Kuhani Mkuu Aliyemhukumu Yesu
    Mnara wa Mlinzi—2006 | Januari 15
    • [Picha katika ukurasa wa 10]

      Yosefu mwana wa Kayafa

      [Picha katika ukurasa wa 10]

      Sanduku la mifupa lililovumbuliwa hivi karibuni

      [Hisani ya Picha katika ukurasa wa 10]

      Ossuary, inscription, and cave in background: Courtesy of Israel Antiquities Authority

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki