Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ukaribishaji-Wageni wa Kikristo Katika Ulimwengu Uliogawanyika
    Mnara wa Mlinzi—1996 | Oktoba 1
    • 15. Ni pindi zipi za pekee huenda zikathibitika kuwa nyakati za furaha kwa watu wa Yehova?

      15 Ingawa Wakristo wa kweli hawafuati desturi zijulikanazo sana wala hawaadhimishi sikukuu na misherehekeo ya kilimwengu, kuna pindi wanapokusanyika pamoja ili kufurahia ushirika wa mmoja na mwenzake. Kwa kielelezo, Yesu alihudhuria karamu ya ndoa katika Kana na akachangia shangwe ya pindi hiyo kwa kufanya muujiza wake wa kwanza huko. (Yohana 2:1-11) Vivyo hivyo leo, watu wa Yehova wanakuwa na nyakati za furaha pamoja kwenye pindi za pekee kama hizo, na miadhimisho na misherehekeo ifaayo huchanga mengi kwenye matukio hayo. Hata hivyo, ni mambo gani yafaayo?

  • Ukaribishaji-Wageni wa Kikristo Katika Ulimwengu Uliogawanyika
    Mnara wa Mlinzi—1996 | Oktoba 1
    • 17. (a) Ni mambo gani yanayoonyesha kwamba ile karamu ya arusi katika Kana ilikuwa na mpango mzuri na ilisimamiwa ifaavyo? (b) Ni nini kinachoonyesha kwamba Yesu alikubali pindi hiyo?

      17 Tusomapo Yohana 2:1-11 (NW), si vigumu kwetu kuona kwamba tukio hilo lilikuwa limepangwa vizuri na kwamba idadi kubwa sana ya wageni ilikuwapo. Hata hivyo, Yesu na wanafunzi wake walikuwa wageni ‘walioalikwa’; wao hawakudoea, ingawa angalau baadhi yao yamkini walikuwa watu wa ukoo wa mkaribishaji-wageni. Twaona pia kwamba kulikuwa na wale waliokuwa “watumishi” na vilevile “mwelekezi” (NW), ambaye angetoa mielekezo juu ya kilichoandaliwa au kufanywa. Yote hayo yaonyesha kwamba tukio hilo lilikuwa na mpango mzuri na lilisimamiwa ifaavyo. Simulizi lamalizia kwa kutaarifu kwamba kwa lile alilofanya kwenye karamu hiyo, Yesu ‘aliudhihirisha utukufu wake.’ Je, angeamua kufanya hivyo kwenye pindi hiyo ikiwa ingekuwa karamu yenye makelele na isiyodhibitiwa? Bila shaka la.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki