-
Mwe na Imani Kama ya Abrahamu!Mnara wa Mlinzi—2001 | Agosti 15
-
-
Adui Ashambulia
16. (a) Kwa nini maneno ya utangulizi ya Mwanzo 14:1 yanaonyesha kwamba jambo baya li karibu kutokea? (b) Kwa nini wafalme wanne wa mashariki walifanya uvamizi?
16 “Ikawa siku za Amrafeli mfalme wa Shinari, na Arioko mfalme wa Elasari, na Kedorlaoma mfalme wa Elamuc na Tidali mfalme wa Goimu, walifanya vita.” Katika Kiebrania cha awali, maneno hayo ya utangulizi (“Ikawa siku za . . .”) yanaonyesha kwamba jambo baya li karibu kutokea na yanaashiria “kipindi cha majaribu kinacholeta baraka.” (Mwanzo 14:1, 2, NW, kielezi-chini) Jaribu hilo lilianza wakati wafalme hawa wanne wa mashariki pamoja na majeshi yao walipofanya uvamizi wao wenye uharibifu huko Kanaani. Walikuwa na lengo gani? Walitaka kukomesha uasi wa miji mitano ya Sodoma, Gomora, Adma, Seboimu, na Bela. Waliishinda miji hiyo, “wakakutana panapo bonde la Sidimu, kwenye Bahari ya Chumvi.” Loti na familia yake waliishi hapo karibu.—Mwanzo 14:3-7.
-
-
Mwe na Imani Kama ya Abrahamu!Mnara wa Mlinzi—2001 | Agosti 15
-
-
c Wakati mmoja wachambuzi walidai kwamba Elamu haukuwa na uvutano kama huo huko Shina na kwamba simulizi kuhusu shambulizi la Kedorlaoma ni la uwongo. Ili kupata habari zaidi juu ya uthibitisho wa akiolojia unaounga mkono simulizi hilo la Biblia, ona gazeti Mnara wa Mlinzi la Julai 1, 1989, ukurasa wa 4-7.
-