-
“Vita Si Yenu Bali Ni ya Mungu”Amkeni!—2000 | Aprili 22
-
-
Katika Julai 4, 1940, kabla tu ya kuanza kwenda kwenye chuo cha sheria, serikali ya Kanada iliwapiga marufuku Mashahidi wa Yehova pasipo onyo.
-
-
“Vita Si Yenu Bali Ni ya Mungu”Amkeni!—2000 | Aprili 22
-
-
Vita ya Ulimwengu ya Pili ilikuwa imepamba moto, na Mashahidi walikuwa wangali chini ya marafuku katika Kanada. Wanaume na wanawake walikuwa wanatiwa gerezani kwa sababu tu ya kuwa Mashahidi wa Yehova. Watoto walikuwa wakifukuzwa shuleni, hata baadhi yao walihamishwa nyumbani kwao. Kwa sababu walikataa kushiriki namna mbalimbali ya ibada ya kitaifa, kama vile kusalimu bendera au kuimba wimbo wa taifa. Profesa William Kaplan, aliyeandika kitabu kinachoitwa State and Salvation: The Jehovah’s Witnesses and Their Fight for Civil Rights, alisema kwamba “Mashahidi walitukanwa hadharani na kushambuliwa na serikali isiyowavumilia na vikundi vya raia wenye uhasama wa peupe ambao walinaswa katika tamaa na uzalendo wa vita.”
Mashahidi walikuwa wanaomba marufuku yaondolewe bila mafanikio. Ghafula, yaliondolewa katika Oktoba 14, 1943. Lakini, Mashahidi walikuwa wangali gerezani na katika kambi za kazi ngumu, bado watoto walizuiwa kujiunga na shule za umma, na bado shirika la Watch Tower Bible and Tract Society na International Bible Students Association, shirika lililomiliki vifaa vyetu huko Toronto yalipigwa marufuku.
Mwishoni mwa mwaka wa 1943, nilisafiri hadi New York pamoja na Percy Chapman, aliyekuwa mwangalizi wa ofisi ya tawi ya Kanada, ili kufanya mashauri na Nathan Knorr, aliyekuwa msimamizi wa Watch Tower Society wakati huo, na Hayden Covington, naibu-msimamizi na mshauri wa kisheria wa Society. Ndugu Covington alikuwa na ujuzi mwingi sana wa kisheria. Hatimaye alishinda kesi za rufani 36 kati ya 45 katika Mahakama Kuu Zaidi ya Marekani.
Hali ikawa nafuu hatua kwa hatua kwa Mashahidi katika Kanada. Jengo la tawi katika Toronto lilirejeshwa mwaka wa 1944, na waliokuwa wakitumikia humo kabla ya marufuku waliweza kurudi. Mahakama kuu ya jimbo la Ontario ilitangaza mnamo mwaka wa 1945 kwamba watoto hawatalazimishwa kushiriki utendaji wanaokataa kwa kudhamiria. Iliamuru kwamba watoto waliofukuzwa shuleni wakubaliwe tena shuleni. Hatimaye, katika mwaka wa 1946 serikali ya Kanada iliwaachilia huru Mashahidi wote kutoka katika kambi za kazi ngumu.
-