-
Msafiri Dhaifu Lakini HodariAmkeni!—1996 | Oktoba 8
-
-
Ingawa baadhi ya vipepeo husemwa kwamba huhamia mbali zaidi kipupwe kianzapo, ni kipepeo-maliki pekee ambaye hufunga safari ndefu wakijua kihususa wanakoenda na kusafiri kwa wingi sana. Uhamaji wa kipepeo-maliki kwa kweli ni ajabu ya kipepeo. Ebu fikiria baadhi ya matimizo yenye kuvutia ya wasafiri hawa hodari.
Safari zao za kutoka Kanada wakati wa vuli na kwenda makao yao ya kipupwe katika California au Mexico ni zaidi ya kilometa 3,200.
-
-
Msafiri Dhaifu Lakini HodariAmkeni!—1996 | Oktoba 8
-
-
Gazeti Canadian Geographic lataarifu: “Kwa wazi, kuna programu fulani ya kijeni yenye kutatanisha sana katika bongo zao ndogo za hali ya chini, labda njia fulani za kusoma mkao wa miale ya jua, kama ambavyo nyuki hufanya, au kusoma uga sumaku wa dunia, ambao yaonekana huongoza ndege. Uwezo wa kutambua halijoto na unyevu hususa waweza kuwasaidia wafikapo mwisho wa safari yao. Lakini kufikia sasa sayansi imeshindwa kupata majibu.”
-
-
Msafiri Dhaifu Lakini HodariAmkeni!—1996 | Oktoba 8
-
-
Mwanasayansi wa Chuo Kikuu cha Toronto David Gibo amegundua kwamba kipepeo-maliki hufanya zaidi ya kupaa na kwenda tu hewani. Yeye aripoti hivi: “Ni lazima vipepeo hawa watumie upepo katika njia ninayofikiri ni zenye werevu zaidi kuliko wanavyofanya bata bukini wanaohama.” Kule kupiga-piga kwa mabawa, kupaa, na kujilisha huruhusu vipepeo-maliki kufika Mexico wakiwa na mafuta ya kuwatosha kupitisha kipupwe na kuanza safari yao ya kurudi kaskazini katika masika. Profesa Gibo asema pia: “Ni kwa kuenda na upepo kunakofanya watimize safari yao ndefu na kufika wakiwa wenye nguvu na wenye afya nzuri.”
-
-
Msafiri Dhaifu Lakini HodariAmkeni!—1996 | Oktoba 8
-
-
Lakini mahali idadi kubwa za kipepeo-maliki walio kaskazini mwa Kanada zilipokuwa zikienda hapakujulikana kwa muda fulani.
-
-
Msafiri Dhaifu Lakini HodariAmkeni!—1996 | Oktoba 8
-
-
Mojayapo mahali pazuri zaidi katika Kanada pa kuona kipepeo-maliki kwa wingi ni katika Hifadhi ya Kitaifa ya Point Pelee, Ontario, ambako wao hujikusanya kwa wingi katika matayarisho ya kuhama kusini. Katika mwisho-mwisho wa kiangazi wao hujikusanya katika mahali pa kusini zaidi pa Kanada, wakingoja kwenye ukingo wa kaskazini wa Ziwa Erie mpaka pepo na halijoto ziwafae kabla ya kuanza safari yao ya kusini kuelekea makao yao ya kipupwe katika Mexico.
-
-
Msafiri Dhaifu Lakini HodariAmkeni!—1996 | Oktoba 8
-
-
Wakianza safari Point Pelee, wao husafiri kisiwa hadi kisiwa wakivuka Ziwa Erie ili kuanza safari ndefu kuvuka bara la Marekani.
-
-
Msafiri Dhaifu Lakini HodariAmkeni!—1996 | Oktoba 8
-
-
Masika hufika, na kipepeo-maliki huwa watendaji tena. Siku ziwavyo ndefu zaidi, hao vipepeo huruka-ruka kwenye jua, wao huanza kujamiiana, na kuanza safari yao ya kurudi kaskazini. Inafikiriwa kwamba wengine waweza kumaliza safari yote ya kurudi, lakini kwa kawaida ni wazao ndio hufika katika milima ya Kanada na kaskazini mwa Marekani wakati wa kiangazi. Vizazi vitatu au vinne vya mayai, mabuu, pupa, na vipepeo hurudi polepole kuvuka kontinenti. Kipepeo wa kike—akiwa amejaza mayai mia moja au zaidi yaliyotungishwa—huruka-ruka kwenye maua ya mwituni na kutaga mayai moja-moja katika upande wa chini wa majani machanga ya milkweed. Na hivyo duru hiyo huendelea na kuendelea, na safari ya kipepeo-maliki ya kurudi makao ya kiangazi huendelea.
-