Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Msiba wa Barafu
    Amkeni!—1998 | Agosti 22
    • Maafa mengine yalizuiwa karibu majuma mawili baadaye wakati ambapo kikundi cha watu 1,889 kilipokusanyika mnamo Januari 24 kwa ajili ya kusanyiko la mzunguko kwenye Jumba la Kusanyiko la Montreal la Mashahidi wa Yehova. Usiku kucha, zaidi ya sentimeta 20 za theluji zilikuwa zimefunika Montreal, na wakati wa programu ya asubuhi ya kusanyiko, madhara yalionekana kwenye kuta na dari. Programu ya alasiri ilifutwa, na waliohudhuria wakaombwa waende nyumbani, wabadili mavazi yao, na kurudi kwenye Jumba la Kusanyiko ili kufanya kazi.

      Katika muda wa saa moja wajitoleaji 300 wakiwa na sepetu, sululu, na vyombo vingine walianza kuondoa theluji kwenye paa kubwa lenye meta za mraba 7,100. Theluji iliyokuwa juu ilipoondolewa, iligunduliwa kwamba katika sehemu fulani barafu ilikuwa na unene unaozidi sentimeta 60! Misumeno ya umeme ilitumiwa kukata barafu katika vipande vya mraba, kisha vikakokotwa mpaka kwenye ukingo wa paa na kuangushwa. Tani zipatazo 1,600 za theluji na barafu ziliondolewa! Baadaye uchunguzi ulifunua kwamba kama matokeo, dari ilijirudisha mahali pake na nyufa katika kuta zikajiziba. Programu ikaanza tena Jumapili asubuhi kwa usalama.

  • Msiba wa Barafu
    Amkeni!—1998 | Agosti 22
    • Msiba ambao ungeweza kutokea ulizuiwa wakati wajitoleaji walipoondoa theluji na barafu kutoka kwenye paa la Jumba la Kusanyiko

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki