-
Mtoto Anapougua KansaAmkeni!—2011 | Mei
-
-
Mtoto Anapougua Kansa
“Nilijihisi nimekata tamaa. Nilihisi ni kana kwamba ulimwengu ulikuwa umepasuka. Nilianza kuomboleza kana kwamba tayari msichana wangu mdogo alikuwa amekufa.”—Jaílton, alipogundua kwamba binti yake alikuwa na kansa.
-
-
Mtoto Anapougua KansaAmkeni!—2011 | Mei
-
-
● Jaílton na Néia “Binti yetu alipokuwa na umri wa miaka miwili na nusu iligunduliwa kuwa ana lymphoblastic leukemia, kansa hatari ya damu inayoharibu chembe nyeupe za damu.”
Matibabu yalichukua muda gani?
“Alitibiwa kwa kemikali kwa karibu miaka miwili na nusu.”
Matibabu hayo yalikuwa na athari gani?
“Alitapika sana na nywele zake zote zikang’oka. Meno yake yakawa meusi. Na akaugua nimonia mara tatu.”
Hilo liliwaathiri jinsi gani?
“Mwanzoni tuliogopa sana. Lakini tulipoona kwamba anapata nafuu, tulianza kuwa na tumaini kwamba atapona. Sasa anakaribia umri wa miaka tisa.”
Ni nini kilichowasaidia kukabiliana na hali hiyo yenye kufadhaisha?
“Bila shaka ni kwa sababu tulimtegemea Yehova Mungu, ambaye ‘alitufariji katika dhiki yetu yote,’ kama Biblia inavyosema kwenye 2 Wakorintho 1:3, 4. Ndugu na dada zetu wa Kikristo walitutegemeza sana. Walituandikia barua zenye kutia moyo, wakatupigia simu, wakasali nasi na pia kwa ajili yetu, na hata wakatusaidia kifedha. Kisha, binti yetu alipohamishwa kwenye hospitali fulani katika jimbo lingine, Mashahidi huko walitupa makao na wakapanga kutupeleka hospitali kwa zamu. Hatuna maneno ya kutosha kueleza shukrani zetu kwa utegemezo wote tuliopata.”
● Luiz na Fabiana “Katika mwaka wa 1992 tuliambiwa kwamba binti yetu alikuwa na aina fulani ya kansa ya ovari ambayo huenea haraka mwilini. Alikuwa na umri wa miaka 11.”
Mwanzoni mlifanya nini mlipopokea habari hizo?
“Hatukuamini. Hatungeweza kukubali kwamba binti yetu alikuwa na kansa.”
Alipata matibabu gani?
“Alifanyiwa upasuaji na kutibiwa kwa kemikali, na matibabu hayo yalituchosha kimwili na kutufadhaisha kihisia. Mara mbili binti yetu aliugua nimonia. Mara ya pili karibu afe. Pia alikuwa na upungufu wa vigandisha-damu, kwa hiyo damu ikaanza kutoka kwenye ngozi na puani. Alipewa dawa za kutuliza hali hiyo.”
Matibabu hayo yalichukua muda gani?
“Alitibiwa kwa miezi sita hivi tangu kansa ilipogunduliwa hadi awamu ya mwisho ya matibabu ya kemikali.”
Binti yenu alihisi namna gani kuhusu ugonjwa huo na matibabu yake?
“Mwanzoni, hakuelewa ni nini kilichokuwa kikiendelea. Daktari alimwambia kwamba alikuwa na ‘mpira mdogo katika tumbo lake ambao ulihitaji kuondolewa.’ Baadaye alipogundua hali si nzuri, aliniuliza, ‘Baba, nina kansa?’ Ilikuwa vigumu sana kwangu kumjibu.”
Mlihisi namna gani mlipomwona binti yenu akiteseka?
“Ni vigumu sana kueleza maumivu ya kihisia tuliyopata. Hebu wazia ukimtazama binti yako mdogo akimsaidia muuguzi kupata mshipa wa damu ili aweze kutiwa kemikali mwilini. Hali ilipokuwa mbaya sana, nilienda chooni kulia na kusali. Usiku mmoja, nilifadhaika sana hivi kwamba nilimwomba Yehova aache nife badala ya binti yangu mdogo.”
Ni nini kilichowasaidia kukabiliana na hali hiyo?
“Jambo kuu ni utegemezo tuliopata kutoka kwa ndugu zetu wa kiroho, ambao baadhi yao walitupigia simu kutoka sehemu mbalimbali za nchi. Ndugu mmoja mpendwa aliniomba nichukue Biblia yangu. Kisha akasoma mistari fulani kutoka katika kitabu cha Zaburi. Mistari hiyo ilitufariji sana kwani wakati huo mimi na mke wangu tulikuwa tukipitia kipindi kigumu sana kwa sababu ya matibabu ya binti yetu.”
● Rosimeri “Binti yangu alikuwa na umri wa miaka minne ilipogunduliwa kwamba alikuwa na lukemia.”
Ulifanya nini ulipopata habari hizo?
“Sikuamini nilichokuwa nikisikia. Nililia usiku na mchana na kumsihi Mungu anisaidie. Binti yangu mkubwa aliumia kihisia alipoona kwamba dada yake alikuwa mgonjwa sana. Ilibidi nimpeleke akaishi na mama yangu kwa muda fulani.”
Binti yako alipata athari gani kutokana na matibabu?
“Matibabu ya kemikali aliyopata kila siku yalifanya awe na upungufu wa damu mwilini, kwa hiyo madaktari walimpa madini ya chuma na pia dawa ya erythropoietin ambayo husaidia kutokeza chembe nyekundu za damu. Upungufu huo wa damu ulinitia wasiwasi kila wakati. Pia alikuwa akizimia mara kwa mara.”
Matibabu hayo yaliendelea kwa muda gani?
“Alitibiwa kwa kemikali kwa muda wa miaka miwili na miezi minne. Katika kipindi hicho, nywele zake zote ziling’oka na akaongeza uzito sana. Lakini kwa kuwa yeye ni mcheshi, aliweza kukabiliana na hali hiyo. Baada ya miaka sita hivi, madaktari walisema kwamba binti yangu hakuwa tena na dalili za ugonjwa huo.”
Ni nini kilichokusaidia kukabiliana na hali hiyo ngumu?
“Mimi na binti yangu tulisali mara nyingi, na tulizungumzia mifano ya Biblia ya watumishi waaminifu wa Mungu waliovumilia majaribu mbalimbali. Pia tulifuata maneno ya Yesu kwenye Mathayo 6:34 kwamba tusihangaikie mambo ya kesho. Pia tulipata msaada kutoka kwa Wakristo wenzetu, kutia ndani ndugu wa Halmashauri ya Uhusiano na Hospitali, na kutoka kwa wahudumu wa kitiba wenye kujali ambao mara kwa mara hushughulika na hali kama yetu.”
-
-
Mtoto Anapougua KansaAmkeni!—2011 | Mei
-
-
[Picha katika ukurasa wa 13]
Néia, Sthefany, na Jaílton
[Picha katika ukurasa wa 13]
Luiz, Aline, na Fabiana
[Picha katika ukurasa wa 13]
Aline na Rosimeri
-