Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Virusi Ambavyo Wanawake Wanapaswa Kujua
    Amkeni!—2005 | Juni 22
    • Jinsi ya Kujua Ikiwa Umeambukizwa

      Ikiwa wewe ni mwanamke, huenda ukajiuliza, ‘Nitajuaje kwamba nimeambukizwa virusi vya HPV?’ Hilo ni swali muhimu kwa kuwa dalili za ugonjwa huo hazijitokezi waziwazi. Kwa hiyo, kama alivyofanya Cristina aliyetajwa mwanzoni mwa makala hii, hatua muhimu ni kufanyiwa uchunguzi wa chembe za mlango wa tumbo la uzazi, yaani, Pap smear, au Papanicolaou smear.c

      Ili kufanya uchunguzi huo, daktari hutoa chembe chache za mlango wa tumbo la uzazi na kuzipeleka kwenye maabara ili zichunguzwe. Uchunguzi huo unaweza kuonyesha ikiwa mtu ameambukizwa, ana uvimbe, au ana chembe zisizo za kawaida. Inaripotiwa kwamba uchunguzi wa Pap smear umepunguza idadi ya watu wanaopatwa na kansa ya mlango wa tumbo la uzazi na vifo vinavyosababishwa na kansa hiyo.

  • Virusi Ambavyo Wanawake Wanapaswa Kujua
    Amkeni!—2005 | Juni 22
    • Mbali na kujifunza kuhusu maadili, wanawake wanapaswa kujua kuhusu ugonjwa huo na kuelewa umuhimu wa kufanyiwa uchunguzi mbalimbali kwa ukawaida kama vile Pap smear.d

  • Virusi Ambavyo Wanawake Wanapaswa Kujua
    Amkeni!—2005 | Juni 22
    • c Uchunguzi huo ulipewa jina la daktari Mgiriki, George N. Papanicolaou, ambaye alivumbua mbinu ya kutia chembe rangi ili kuzichunguza.

  • Virusi Ambavyo Wanawake Wanapaswa Kujua
    Amkeni!—2005 | Juni 22
    • d Kulingana na Taasisi ya Kitaifa ya Kansa ya Marekani, uchunguzi huo unapaswa kufanyiwa mtu anapofikia umri wa miaka 18 au anapoanza kufanya ngono.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki