Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Sehemu ya 1—Kuwa Mashahidi Hadi Sehemu ya Mbali Zaidi Sana ya Dunia
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • Joseph Brathwaite, aliyekuwa katika Guiana ya Uingereza wakati aliposaidiwa kuelewa kusudi la Mungu, aliondoka kwenda Barbados katika 1905 ili kutumia wakati wake wote katika kufundisha watu huko. Louis Facey na H. P. Clarke, waliosikia habari njema wakati walipokuwa wakifanya kazi katika Kosta Rika, walirudi Jamaika katika 1897 ili kushiriki imani yao mpya waliyoipata miongoni mwa watu wao wenyewe. Wale waliokubali kweli huko walikuwa wafanyakazi wenye bidii. Katika 1906 pekee, kikundi hicho katika Jamaika kiligawanya trakti zipatazo 1,200,000 na vipande vingine vya fasihi. Mfanyakazi mwingine mhamaji, aliyejifunza kweli katika Panama, alipeleka ujumbe wa tumaini katika Grenada.

  • Sehemu ya 1—Kuwa Mashahidi Hadi Sehemu ya Mbali Zaidi Sana ya Dunia
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • Ili kufungua nchi zaidi za Karibea kwa kazi ya kuhubiri kweli ya Biblia na kupanga mikutano ya ukawaida kwa ajili ya funzo, Ndugu Russell alituma E. J. Coward kwenda Panama katika 1911 na kisha kwenye visiwa. Ndugu Coward alikuwa msemaji mwenye mkazo na mwenye kupendeza, na wasikilizaji ambao mara nyingi walifikia idadi ya mamia walisongamana kusikia hotuba zake zenye kukanusha fundisho la moto wa helo na kutokufa kwa nafsi ya kibinadamu, pia akisimulia juu ya wakati ujao mtukufu kwa ajili ya dunia. Alisonga toka mji mmoja kwenda ufuatao, na toka kisiwa kimoja hadi kingine—St. Lucia, Dominika, St. Kitts, Barbados, Grenada, na Trinidad—akifikia watu wengi iwezekanavyo. Pia alitoa hotuba katika Guiana ya Uingereza. Alipokuwa Panama, alikutana na W. R. Brown, ndugu kijana Mjamaika mwenye bidii sana, ambaye baada ya hapo alitumika pamoja na Ndugu Coward katika visiwa kadhaa vya Karibea. Baadaye Ndugu Brown alisaidia kufungua kazi katika mashamba mengine.

      Katika 1913, Ndugu Russell mwenyewe alitoa hotuba katika Panama, Kuba, na Jamaika. Majumba mawili yalijaa pomoni kwa ajili ya hotuba ya watu wote aliyotoa katika Kingston, Jamaika, na bado watu 2,000 hawakuruhusiwa kuingia kwa kutokuwa na nafasi. Vyombo vya habari vilitaja uhakika wa kwamba msemaji hakusema lolote juu ya pesa na michango haikukusanywa.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki