Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Wadudu Wanaoliwa—Mlo Ambao Hatutausahau
    Amkeni!—2012 | Juni
    • Aina mbalimbali za viwavi huliwa nchini kote. Tulialikwa kufurahia viwavi vya Imbrasia. Nondo mkubwa mwenye rangi ya kahawia hutaga mayai yake kwenye mti wa mbambakofi. Baada ya mayai kuanguliwa, wanakijiji hukusanya viwavi vinavyotoka na kuviosha. Kisha viwavi hivyo huchemshwa pamoja na nyanya, vitunguu, na vikolezo vingine ikitegemea kile ambacho familia ingependa kula. Huenda baadhi ya viwavi hivyo vikakaushwa kwa njia mbalimbali ili vihifadhiwe. Vinaweza kuhifadhiwa kwa miezi mitatu hivi ili viliwe baadaye.

  • Wadudu Wanaoliwa—Mlo Ambao Hatutausahau
    Amkeni!—2012 | Juni
    • Ingawa viwavi ni wadogo, kiwango chao cha virutubisho ni chenye kustaajabisha. Kulingana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, kiasi cha protini kilicho katika viwavi waliokaushwa ni mara mbili zaidi ya kile kilicho katika nyama ya ng’ombe. Wataalamu wa vyakula wamegundua kwamba wadudu ni chanzo cha lishe bora katika nchi zinazoendelea.

      Ikitegemea mtu anakula aina gani ya viwavi, gramu 100 tu ya viwavi inatosha kumwandalia mwanadamu kiasi cha madini muhimu ambayo anahitaji kila siku mwilini kama vile kalisi, chuma, magnesi, fosforasi, potasiamu, na zinki, pamoja na vitamini nyingi. Pia, unga uliotengenezwa kutokana na viwavi unaweza kupikwa kama uji ambao huwa ni lishe bora kwa watoto wenye utapiamlo.

  • Wadudu Wanaoliwa—Mlo Ambao Hatutausahau
    Amkeni!—2012 | Juni
    • Ella alirudi kutoka jikoni akiwa na mlo mkuu ambao ulikuwa ukifuka moshi ulionasa uangalifu wa kila mmoja wetu. Mezani tulikuwa tumeketi na wenyeji wanane wa Afrika ya Kati ambao walitabasamu kwa uchangamfu, na mbele yetu kulikuwa na bakuli mbili kubwa zilizojazwa viwavi. Kwa kuwa tulikuwa wageni, sisi ndio tuliopewa heshima ya kupakuliwa kwanza na tulitiliwa chakula kingi.

  • Wadudu Wanaoliwa—Mlo Ambao Hatutausahau
    Amkeni!—2012 | Juni
    • [Picha katika ukurasa wa 27]

      Makongo au viwavi ambao hawajapikwa

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki