Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Umati Mkubwa Wenye Watu Wengi Sana
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 8 Pasipo shaka, hayo matawi ya mitende na vilio vya kuchachawa pia vinamkumbusha Yohana ile Sikukuu ya Vibanda ya kale ya Israeli. Kwa ajili ya sikukuu hii Yehova aliamuru: “Na ni lazima nyinyi mjichukulie kwa ajili yenu wenyewe katika siku ya kwanza tunda la miti mizuri sana, na matagaa ya mitende na matanzu ya miti yenye matawi na mipopla ya bonde la mvo, na ni lazima nyinyi mshangilie mbele za Yehova Mungu wenu siku saba.” Matawi ya mitende yalitumiwa kuwa alama ya kushangilia. Vibanda vya muda vilikuwa kikumbusha kwamba Yehova alikuwa amewaokoa watu wake kutoka Misri, waishi katika mahema katika jangwa. “Mkazi mgeni na mvulana asiye na baba na mjane” walishiriki hii sikukuu. Waisraeli wote walipaswa ‘wawe si kitu ila wenye kujawa na shangwe.’—Walawi 23:40; Kumbukumbu 16:13-15, NW.

  • Umati Mkubwa Wenye Watu Wengi Sana
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 9. Umati mkubwa unajiunga katika kilio gani cha shangwe?

      9 Basi, inafaa kwamba, umati mkubwa, ingawa si sehemu ya Israeli wa kiroho, upungepunge matawi ya mitende kwa kuwa wanaonyesha kwa shangwe na asante kwamba ushindi na wokovu hutoka kwa Mungu na Mwana-Kondoo kama Yohana anavyoona hapa: “Nao hufuliza kulia kwa sauti kubwa, kusema: ‘Wokovu wetu ni kwa Mungu wetu, ambaye ameketi juu ya kiti cha ufalme, na kwa Mwana-Kondoo.’” (Ufunuo 7:10, NW)

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki