Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Useja wa Kidini Ni Takwa kwa Wahudumu Wakristo?
    Amkeni!—1998 | Juni 8
    • Katika wakati fulani uliopita, dini kadhaa zilizo mashuhuri zimechukua useja kuwa takwa kwa wahudumu wao. Useja wa kidini umekuwa chapa ya Ukatoliki zaidi ya dini nyingine yoyote katika Jumuiya ya Wakristo. Leo, kuna ubishi mkubwa juu ya useja wa Kikatoliki. Gazeti The Wilson Quarterly lilionelea kwamba “uchunguzi mwingi uliofanywa katika miongo ya karibuni umefikia mkataa kwamba useja wa kulazimishwa, takwa la makasisi Wakatoliki tangu karne ya 12, ndio chanzo cha matatizo ya kanisa katika kusajili na kuhifadhi makasisi.” Kulingana na mwanasoshiolojia Richard A. Schoenherr, “mambo ya hakika ya historia na badiliko la kijamii yanapinga dhana inayoruhusu waseja wa kiume tu katika ukasisi wa Kikatoliki.” Biblia ina maoni gani kuhusu useja wa kidini?

  • Je, Useja wa Kidini Ni Takwa kwa Wahudumu Wakristo?
    Amkeni!—1998 | Juni 8
    • Yesu Kristo alisema kuwa “Hekima huthibitishwa kuwa yenye uadilifu kwa kazi zayo.” (Mathayo 11:19) Upumbavu wa kugeuka kutoka kwenye viwango vya Mungu umethibitishwa na kazi zake au matokeo yake. Mwandishi David Rice aliwahoji makasisi wengi kotekote ulimwenguni juu ya habari ya useja wa lazima. Baadhi ya wale aliozungumza nao walisema: “Unabaki katika ukasisi, unajaribu kuwasaidia watu kwa kadiri uwezavyo, na kwa busara upatikane kwa utayari kwa wanawake wa kidini wanaokutamani na ambao wako tayari kufanya ngono nawe.”

      Akinukuu Mathayo 7:20, Rice ataarifu: “‘Kwa matunda yao mtawatambua,’ Yesu alisema.” Kisha aeleza juu ya msiba ambao umetokana na useja wa lazima: “Matunda ya useja wa kulazimishwa ni yale maelfu ya wanaume wanaoishi maisha maradufu, maelfu ya wanawake wanaoishi maisha yaliyoharibiwa, maelfu ya watoto waliokataliwa na baba zao makasisi, kwa kuongezea makasisi wenyewe ambao huteseka kihisia-moyo kwa sababu ya hali hii.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki