-
Kemikali—Je, Ni Rafiki na Adui?Amkeni!—1998 | Desemba 22
-
-
“Majaribio yameonyesha kwamba,” yasema ripoti katika gazeti Discover, “PCB zinapotumiwa wakati fulani hususa wakati wa ukuzi zaweza kubadili kasa na mamba wa kiume kuwa wa kike au ‘wawe kati ya jinsia zote.’”
-
-
Kemikali—Je, Ni Rafiki na Adui?Amkeni!—1998 | Desemba 22
-
-
Watoto waliozaliwa na wanawake waliomeza mafuta ya makapi ya mchele yaliyokuwa na PCB katika Japani miaka kadhaa iliyopita, “walipatwa na ukuzi wa polepole wa kimwili na wa kiakili, matatizo ya tabia kutia ndani kutotenda sana na kutenda kupita kiasi, uume ulio mdogo kupita kiasi, na kiwango cha akili kilichopungua pointi tano chini ya wastani,” laripoti gazeti Discover. Uchunguzi uliofanyiwa watoto walioishi katika maeneo yaliyo na PCB ya kiwango cha juu katika Uholanzi na Amerika Kaskazini ulifunua madhara makali yaliyo na matokeo sawa na haya kwa ukuzi wao wa kimwili na wa kiakili.
-