Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ukosefu wa Makao—Tatizo la Ulimwenguni Pote
    Amkeni!—2005 | Desemba 8
    • Kulingana na ripoti iliyotolewa miaka michache iliyopita katika gazeti The Economist, maelfu ya watoto wa mitaani walikuwa wakiishi katika vijia vyenye uvundo vinavyoelekea kwenye mabomba ya maji machafu au kwenye mfumo wa kupasha jiji joto chini ya barabara za jiji la Ulaanbaatar, Mongolia. Ingawa Wamongolia walishtuka kusikia kuhusu watoto hao wasio na makao, wengi wao walikata kauli kwamba hali hiyo ilitokea “kwa sababu watu ni wavivu sana hivi kwamba hawawezi kuwatunza watoto wao,” lilisema jarida hilo.

      Katika sehemu nyingine ya ulimwengu, watoto wa mitaani huuawa na vikundi vya kulinda usalama vinavyochukua sheria mikononi mwao. Kwa nini? Kichapo fulani cha Umoja wa Mataifa kinaeleza hivi: “Huko Amerika Kusini, wafanyakazi wengi wa idara ya mahakama, polisi, vyombo vya habari, wafanyabiashara, na jamii kwa ujumla wanaamini kwamba watoto wa mitaani ni tisho kwa maadili ya jamii iliyostaarabika.” Kichapo hichohicho kinasema: “Inaripotiwa kwamba kwa wastani watoto watatu wa mitaani huuawa kila siku katika jimbo la Rio de Janeiro.”

  • Ukosefu wa Makao—Tatizo la Ulimwenguni Pote
    Amkeni!—2005 | Desemba 8
    • [Picha katika ukurasa wa 2, 3]

      Watoto fulani wasio na makao huishi ndani ya shimo hili la maji machafu

      [Hisani]

      Jacob Ehrbahn/Morgenavisen Jyllands-Posten

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki