Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Daraka Lako Ukiwa Mzazi
    Amkeni!—2004 | Oktoba 22
    • Tenga Wakati wa Kumfundisha Mtoto

      Kufundisha ni sehemu muhimu ya kuzoeza na kulea watoto ili wawe na sifa nzuri. Wazazi wengi hutenga wakati kila siku ili kuwasomea watoto wao kwa sauti. Hilo huwapa nafasi ya kuwafundisha watoto wao tabia nzuri na maadili yanayotegemea maagizo ya Muumba wetu. Biblia inasema kwamba ‘tangu utoto mchanga’ mwalimu mwaminifu na mishonari aliyeitwa Timotheo ‘aliyajua maandishi matakatifu.’—2 Timotheo 3:15.

      Kumsomea mtoto wako kunaweza kuchochea ubongo wake. Ni muhimu mtoto asomewe na mtu aliye chonjo na anayejali. Profesa wa elimu, Linda Siegel anatoa tahadhari hii kuhusu habari ambayo mtoto anapaswa kusomewa: “Inapaswa impendeze mtoto.” Pia, jitahidi kumsomea wakati uleule kila siku. Kwa kufanya hivyo, mtoto atakuwa akitarajia kwa hamu kusomewa.

  • Daraka Lako Ukiwa Mzazi
    Amkeni!—2004 | Oktoba 22
    • Jitihada Zinazofanikiwa

      Baba mmoja anayeitwa Fred alimsomea binti yake kwa ukawaida kabla ya kulala tangu akiwa mchanga. Baada ya muda, alitambua kwamba binti yake anakumbuka hadithi nyingi, anafuatana naye anaposoma, na kupatanisha maneno na sauti. Chris pia ni mzazi mwingine aliyejitahidi sana kuwasomea watoto wake. Alijitahidi kusoma habari tofauti-tofauti. Watoto walipokuwa wachanga sana, alitumia picha zilizomo katika vitabu kama vile Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia kufundisha masomo ya kiadili na ya kiroho.b

      Mbali na kuwasomea watoto, wazazi fulani huwahusisha watoto wao katika shughuli mbalimbali kama kuchora, kupaka rangi, kucheza muziki, na kutembelea maeneo mbalimbali kama vile mbuga za wanyama. Wazazi wanaweza kutumia pindi hizo kufundisha na kukazia kanuni za maadili na tabia njema ndani ya mioyo na akili ya mtoto.

  • Daraka Lako Ukiwa Mzazi
    Amkeni!—2004 | Oktoba 22
    • [Sanduku/Picha katika ukurasa wa 10]

      Madokezo Kuhusu Kuwasomea Watoto Wako

      ◼ Sema kwa njia inayoeleweka wazi na utamke maneno vizuri. Mtoto hujifunza lugha kwa kuwasikiliza wazazi wakiongea.

      ◼ Waonyeshe watoto kwa kidole na utaje majina ya watu na vitu vinavyotajwa katika hadithi mnayosoma.

      ◼ Mtoto anapoendelea kukua chagua vitabu vinavyofaa mahitaji yake ya wakati huo.

      [Hisani]

      Source: Pediatrics for Parents

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki