-
Sababu kwa Nini Dini ya Kilimwengu ItaishaMnara wa Mlinzi—1996 | Aprili 15
-
-
7. Mashahidi wa Yehova walifunuaje makasisi wa Jumuiya ya Wakristo zaidi ya miaka 50 iliyopita?
7 Zaidi ya miaka 50 iliyopita, katika kijitabu kiitwacho Religion Reaps the Whirlwind, Mashahidi wa Yehova walifunua kujiingiza kwa Jumuiya ya Wakristo katika siasa.a Yale yaliyosemwa wakati huo yatumika kwa nguvu iyo hiyo leo: “Uchunguzi wenye kufuatia haki wa mwenendo wa makasisi wa kidini wa dini zote utafunua kwamba viongozi wa kidini wa ‘Jumuiya ya Wakristo’ wanashiriki kwa upendezi mwingi katika siasa za ‘ulimwengu huu mwovu wa sasa’ nao wanajiingiza katika mambo ya kilimwengu.” Wakati huo Mashahidi walimchambua vikali Papa Pius 12 kwa ajili ya mikataba aliyofanya pamoja na Hitler Mnazi (1933) na Franco Mfashisti (1941), na pia hali ya papa kubadilishana mabalozi na taifa chokozi Japani katika Machi 1942, miezi michache tu baada ya shambulio baya la Pearl Harbor.
-
-
Sababu kwa Nini Dini ya Kilimwengu ItaishaMnara wa Mlinzi—1996 | Aprili 15
-
-
10. Ni taarifa gani ya wazi iliyotolewa katika 1944?
10 Kama kijitabu Religion Reaps the Whirlwind kilivyouliza katika 1944, ndivyo sisi pia twauliza: “Je, tengenezo lolote lifanyalo mikataba na mamlaka za kilimwengu na kushiriki kabisa katika mambo ya kisiasa ya ulimwengu huu, litafutalo kutumia na kupata ulinzi kutokana na ulimwengu huu . . . laweza kuwa kanisa la Mungu au kumwakilisha Kristo Yesu duniani? . . . Kwa wazi, wanadini wote wenye miradi sawa pamoja na falme za ulimwengu hawawezi kuwakilisha ufalme wa Mungu kupitia Kristo Yesu.”
-