-
Kuhuisha Mashahidi WawiliUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Na maiti zao zitakuwa katika njia pana ya jiji kubwa ambalo kwa maana ya kiroho huitwa Sodoma na Misri, ambako pia Bwana yao alitundikwa kwenye nguzo.
-
-
Kuhuisha Mashahidi WawiliUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Lakini hili “jiji kubwa” lilikuwa nini?
22. (a) Ni nini jiji kubwa? (b) Vichapo vya umma vilijiungaje na viongozi wa kidini katika kushangilia juu ya kunyamazishwa kwa mashahidi wawili? (Ona kisanduku.)
22 Yohana anatupa sisi madokezo fulani. Yeye anasema kwamba Yesu alitundikwa kwenye nguzo huko. Hivyo mara moja sisi tunafikiria Yerusalemu. Lakini yeye anasema pia kwamba hilo jiji kubwa linaitwa Sodoma na Misri. Basi, Yerusalemu halisi liliitwa Sodoma wakati mmoja kwa sababu ya mazoea yalo machafu. (Isaya 1:8-10; linga Ezekieli 16:49, 53-58.) Na Misri, ile serikali ya ulimwengu kubwa ya kwanza, nyakati nyingine huonekana ikiwa picha ya huu mfumo wa mambo wa ulimwengu. (Isaya 19:1, 19; Yoeli 3:19) Kwa sababu hiyo, jiji hili kubwa ni picha ya “Yerusalemu” lililochafuliwa ambalo hudai kuabudu Mungu lakini ambalo limekuwa chafu na lenye dhambi, kama Sodoma, na sehemu ya huu mfumo wa wambo wa ulimwengu wa kishetani, kama Misri. Ni picha ya Jumuiya ya Wakristo, ambayo ni kisawe cha Yerusalemu lisilo jaminifu, tengenezo ambalo washiriki walo walikuwa na sababu kubwa sana ya kushangilia wakati waliponyamazisha ile kazi sumbufu ya mashahidi wawili ya kuhubiri.
-